Maiti nyengine tano za ajali ya meli ya Spice Islanders wamepatikana eneo la Shimoni Mombasa na kulazimka kuzikwa kwenye eneo hilo kutokana na hali zao.

Kwa mujibu wa taarifa wa balozi mdogo wa Tanzania nchini Kenya Yahya Haji Jecha amesema kuanzia jana maiti zimeanza kupatikana eneo la shimoni Mombasa.

Amesema kati ya maiti hizo nne ni za wanaume na moja ni ya mwanamke ambapo maiti hizo zimedaiwa kuwa zimeharika sana ambazo zisingeweza kusafirishwa

Katika hatua nyingine

Kazi za ukozi za kuipata miili mingine kutoka kwenye meli ya Spice Islander iliyozama mwishoni mwa wiki huko Nungwi imesitishwa kwa muda kutoka na hali mbaya ya hewa.

Taarifa kutoka Nungwi zinasema wapiga mbizi wa ndani na wale kutoka Afrika ya kusini wamesitisha kwa muda shguhuli za ukozi kutokana na bahari kuchafuka.

Wakati huo huo usafiri wa baharini kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam umetatizika kutokana na vyombo vya usafiri kuwa kidogo baada ya kutokea ajali ya meli ya Spice Islander.

Hata hivyo nauli za vyombo hivyo zimeripotiwa kupanda

Advertisements