Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Moh’d Shein, amesema huu sio wakati wa kulaumiana na kushtumiana kutokana na Msiba mkubwa uliolipata Taifa kwa kupoteza mamia ya Wananchi kwa kuzama Meli ya Mv, Spice Islandar.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa mkoa wa Kusini Pemba amewataka wananchi kuwa na subira na mshikamano juu ya tukio hilo huku serikali ikiendelea na juhudi za uokozi na uchunguzi wa ajali hiyo.

Dr. Shein amesema msiba huo utabaki historia kutokea katika Visiwa vya Zanzibar tangu kuanza kwa Safari za Meli katika Karne zilizopita.

Amesema msiba huo sio wa Wazanzibar peke bali ni wa Taifa zima la Tanzania kwa vile kila mmoja umemgusa kwa namna moja ama nyengine.

Dk. Shein aliwataka Wananchi wa Zanzibar, kuzidi kushirikiana na kusaidiana na kuonesha utulivu kama waliouonesha katika kipindi cha kutokea ajali ya meli ya Mv Spice Islander.

kwa Mtihani huo kwani yote yaliotokea ni muandiko wa Mwenyeezi Mungu Pekee.

 

Alifahamisha kuwa Serikali zote mbili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano kwa pamoja zilishirikiana na Wananchi mbali mbali ilikuona wanakabiliana na Janga hilo kwa Uokozi wa Watu na kuwazika wale wote walifariki Dunia kila mmoja na Kaburi lake,

 

“ Tulizika maiti zote huko Kama Unguja , kwa vile hatukuwa na namna nyengine kwani Maiti wa maji ya bahari haekeki na Uwezo wa Chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Mnazi Mmoja hakina Uwezo mkubwa kwa wakati mmoja na wale maiti walikuwa wengi.” Alieleza Dk, Shein.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk, Ali Moh’d Shein, alieleza kuwa Serikali imejifunza mengi kutokana na Msiba  huo , na itajitahidi kuona suala kama hilo halitokei tena .

 

Aliwahakikishia Wananchi kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imeazimia kuunda Tume maalumu ilikuchunguza Chanzo cha ajali hiyo , na kuchukuwa ripoti ya uchunguzi huo na hatimae kuchukuwa hatua bila ya upendeleo wala kumuonea mtu.

 

“ Tume tutakayoiunda tutaitangaza haraka sana katika saa zijazo na itafanya kazi bila woga na bila ya kumuonea mtu yoyote” alisema Dk Shein.

 

Aliendelea kusema kuwa kwa kusaidiana na Wahisani na Wafanyabiashara mbali mbali , Serikali imejiandaa kukabiliana na hali kama hiyo kwa kuwataka Wafanya biashara kuekeza katika usafiri wa Baharini kwa kutafuta Meli kubwa itakayo ondowa shida ya usafiri kati ya Pemba na Unguja.

 

“ Pale Serikali itakapo kuwa na uwezo itafanya juhudi ya kumiliki Meli yake wenyewe , hapo siku za nyuma srikali ilikuwa ikimiliki meli mbili mbili, kubwa na ndogo…..ilikuwa na usafiri wa uhakika kwa Wananchi wa Unguja na Pemba”alisema Dk. Shein.

 

Alieleza kuwa pamoja na Serikali kufanya wajibu wake mbali mbali , lakini haija sita kufanya hivyo na inaungana na Wananchi wa Pemba , kwa mtihani huo na amewataka kuwa na subra kwani liliandikwa na Allha halina budi kufanyika .

 

Hivyo  aliwashukuru Watendaji wakuu wa Serikali na Taasisi mbali mbali kwa ujumla kwa kazi kubwa waliochukuwa za kukabiliana na Janga hilo kubwa na nchi ikiwa iko katika hali ya Utulivu.

 

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa srikali imejifunza mambo mengi katika tukio hilo na kueleza lengo lake hivi sasa la kujipanga vizuri huku kukiwa na mashirikiano mazuri pamoja na ahadi mbali mbali za kuunga mkono juu ya jambo hilo kutoka kwa washirika wa maendeleo katika kuweka mikakati zaidi.

 

Nao wananchi na viongozi hao walisifu juhudi za serikali chini ya uongozi wa Dk Shein katika kukabiliana na tukio hilo.

 

Aidha, walieleza kuwa wanaungana na Rais kueleza kuwa huo ni msiba kutoka kwa Allah na kueleza kuwa kama Qur-an na hadithi za Mtume zinavyosisitiza subira basin a wao wamo katika kutekeleza amri hiyo ya Mola wao na Mtume wao Muhammad S.A.W.

 

Kwa mujibu wa uongozi wa Wilaya ya Mkoani ulieleza kuwa watu waliofariki ni 31 na 4 waliokolewa na kwa Wilaya ya Mkoani ni 146 walifariki ambapo kwa Shehia ya ziwani peke yake waliofariki ni 56

Advertisements