Makamo wa pili wa rais Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mitaji na maendeleo ya kijamii Robert Shumake yenye makao makuu yake jimboni Michigan.

Zanzibar imeshauriwa kuangalia njia za kuwatumia vyema Wataalamu  Wazawa  walioko nje ya Nchi  ili kuharakisha kasi ya Maendeleo ya Jamii .

Ushauri huo umetolewa na Kiongozi wa Wazanzibari waliopo Nchini Marekani ambao wako katika hatua za mwisho kuandaa Jumuiya itakayoitwa Zanzibar Diascora Organization Dr. Omar Haji Ali wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozo Seif Ali Iddi kwenye Hoteli ya Crown Plaza Mjini Washington DC. Nchini marekani.

Dr. Omara alimueleza Balozi Seif kwamba lengo la Jumuiya hiyo ni kuunganisha nguvu kati yao na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuona kwamba uwepo wao nje ya Zanzibar unaleta faida  kwa Jamii yote.

Alisema hivi sasa wanakamilisha taratibu za kuwaunganisha wenzao wa miji tofauti ili ifikapo Januari mwakani Jumuiya yao ianze kazi rasmi.

“ Tumefanya utafiti na kugundua Wapo Wazanzibari wengi wenye sifa na uwezo mkubwa kitaaluma ambao wanaweza  kuitumia na kusaidia nyumbani  ”. Alisema Dr. Omar.

Alisisitiza kwamba  taratibu zinaandaliwa  za akuwaunganisha Wazanzibari wengi walioko katika Jumuiya za Uingereza na Canada  kwa ania ya kuwa na kiungo muhimu kati yao na Zanzibar hasa katika  maeneo ya Uwekezaji na Uatafiti katika Sekta tafauti.

Alisema kuanzishwa kwa mawasiliano ya moja kwa moja  yatatoa fursa kwa wenye nia ya kusaidia kupitia jumuiya hiyo.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi  ameipongeza azma yan Jumuiya hiyo ya Zanzibar Diascora Organization  na kuahidi kuipa Baraka.

Balozi Seif  alisema  Serikali inaunga mkono vikundi vya Diascora na kuvitaka kuwa karibu na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania.

“ Serikali ya SMZ tayari imeshaundan Idara inayosimamia Diascora kwa lengo la  kuwaunganisha wazawa walioko nje ya Nchi. Hivyo tutahakikisha mnakuwa na mawasiliano ya karibu na Taasisi hii “ Alisema Balozi Seif Ali Iddi.

 Wakati huo huo

Mamlaka ya Mitaji na Mendeleo ya Jamii ya wa Michigan Nchini Marekani imekubali kuisaidiAZanzibarkatika masuala ya Elimu, Afya na Mazingira.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bwana Robert  Shumake ametoa kauli hiyo wakati wa mazungumao yake na makamu wa Pili wa Rais waZanzibarBalozi Seif Ali Iddi mwishoni mwa ziara yake  Nchini Marekani.

Bw. Shumake ambaye tayari ameshakutana na Uongozi wa Benki ya Watu waZanzibar  PBZ ambao umenambatana na Balozi Seif katika ziata hiyo mamlaka hiyo inajitayarisha kuongeza misaada yake kwaTanzaniaikiwemoZanzibar.

“ Tumeshatoa misaada  ya vifaa vya elimu kwa Nchi za Bara la Afrika ikiwemoEthiopianaTanzaniakatika skuli za Mkoa wa Kilimanjaro” Alisema Bwana Shumake.

Alisisitiza kuwa Mamlaka yake imekuwa ikitoa fursa za kudhamini masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa Afrika wenye mazingira magumu.

Bwana Shumake alisema utafiti uliofanywa na Mamlaka yake umegundua watoto wengi wa Bara la afrika wanashindwa kuendelea na Masomo ya juu kutokana na kukabilkiwa na umaskini uliokithiri.

Alimueleza Balozi Seif kwamba bado wanaangalia uwezekano wa kutoa huduma katika sekta za Kilimo ikilenga zaidi vijana ambao kundi kubwa linakosa ajira na kujikimu kimaisha.

Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ameipongeza Mamlaka hiyo kwa uwamuzi wake wa kusaidia huduma za kijamii.

Balozi Seif alisema Familia nyingi  hasa za kiafrika  zimekuwa zinakosa huduma  za kijamii na kukumbwa na maradhi.

Advertisements