Hamad Rashid

Baadhi ya wananchi wa jimbo la Wawi kisiwani Pemba wameanza kugawanyika kutokana na maamuzi yaliotolewa na baraza kuu la chama cha wananchi CUF ya kumfukuza uanachama mbunge wa jimbo hilo Hammad Rashid Mohammed.

        Wakizungunza na Zenji Fm radio wananchi wanaopinga hatua hiyo wametishia kuandamana na kufikisha malalamiko yao mahakamani.

        Wamesema hawakubaliani na uwamuzi huo kwa vile wananchi wa jimbo hilo  hawakushirikishwa hata kwenye mkutano wa hadhara kuelezwa maamuzi ya baraza hilo.

        Wananchi wengine wanauonga mkono uwamuzi huo nao wamedai kuandamana ili kuunga mkono uwamuzi wa baraza hilo.

        Jeshi la polisi mkoa wa kusini Pemba tayari limeshatoa kibali cha kuruhusu kufanyika maandamano hayo.

        Hamad Rashid na wenzake wannne walifukuzwa uanachama wa chama cha CUF kwa madai ya kutaka kukivuruga chama hicho kufuatia kampeni yake ya kutaka kugombea nafasi ya ukatibu mkuu ambayo kwa sasa inashikiliwa na malim Seif Sharif Hamad.

Advertisements