Baadhi ya watu walionusurika katika jali ya meli ya Spice Islander

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema itawachukulia hatua za kinidhamu na kuwahamishia nafasi za kazi viongozi waliohusishwa na uzembe uliosababisha kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander Septemba mwaka jana.

Akiwasilisha ripoti ya tume ya uchunguzi ya kuzama kwa meli hiyo kwa vyombo vya habari, katibu mkuu kiongozi na baraza la mapinduzi Abdulhamid Yahya Mzee amesema serikali imechukua uwamuzi huo kama ni hatua za awali za kinidhamu kwa viongozi hao.

Amewataja viongozi watakaondolewa kwenye sehemu za kazi na kuhamishiwa sehemu nyingine ni mkurugenzi wa shirika la bandari Mustapha Aboud Jumbe kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama bandarini.

Maafisa wengine ni mkuu wa kituo cha usimamizi wa usalama wa shirika la bandari Usawa Khamis Said, kamimu mdhibiti wa bandari ya Malindi Sarboko Makarni Sarboko, askari wawili walikuwa zamu, afisa mkuu wa meli ya Spice Islander, mabaharia na fundi mkuu wa meli hiyo.

Aidha Mzee amesema waliotajwa na tume hiyo kwa kuchukuliwa hatua za kisheria na kupelekwa mahakamani serikali imewakabidhi watendaji hao kwa polisi na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka.

Amewataka watendaji hao ni mkurugenzi mkuu wa malaka ya usafiri baharini, Haji Vuai Ussi, Mrajisi wa Meli Abdala Mohammed Abdala, mkaguzi wa meli Juma Seif Juma, afisa usalama Simai Nyange Simali.

Wengine ni afisa usafirishaji wa shirika la Bandari Hassan Mussa Mwinyi, wanahisa watatu wa kampuni ya Visiwani Shipping inayomiliki meli na wanahisa wengine wawili kutoka kampuni ya Alhubra Marine Service.

Weingine ni hahodha wa meli Kapteni Said Abdala Kinyanyite, wasimamizi watatu wa uingiaji wa kwenye meli, maafisa wa bodi ya mapato waliokuwepo dhamu.

Watendaji hao watafikishwa mahakamani kwa madai ya kuvunja sheria na kanuni za usalama baharini ikiwemo kuruhusu meli kufanya safari ikiwa haiko salama, na kupakia idadi kubwa ya abiria.

Kuhusu ulipaji wa fidia Mzee amesema utafanywa na wamiliki wa meli hiyo, kwa abiria waliokufa watalipwa asilimia 80,  waliopata ulemavu asilimia 75 na walionusurika asilimia 50 ya kima cha chini cha mshahara kwa kipindi cha miezi 80.

        Kwa upande wa mabaharia na wenye mizigo wahusika hao watafuatilia haki zao mahakami kutokana na kampuni hiyo haikuwa na bima ya mizigo.

        Aidha amesema ripoti hiyo pia imetaja tatizo la rushwa ambalo limechangia kutokea kwa ajali hiyo kwa kuwepo uhusiano wa karibu baina ya watendaji wa bandari na wamiliki wa meli.

Kuhusu suala la kuwajibika kwa waziri wa masiliano na miundo mbinu Hamad Masou amesema ni hiari yake kama ataamuwa kuwajibika kwa kujiuzulu au la.

Kwa muibu wa ripoti ya kamatu ya uchunguzi ya kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander katika mkondo wa Nungwi meli hiyo ilikuwa na zaidi ya abiria elfu mbili na 400 wakati uwezo wake ni kupakia abiria 600.

Advertisements