Waziri wa kazi, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na ushirika

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeongeza mshahara wa kima cha chini kwa sekta binafsi kutoka shilingi elfu 70 hadi shilingi laki moja na elfu 45 kwa mwezi sawa na ongezeko la asimia 107.14.

        Akitangaza ongezeko hilo kwa wandishi wa habari, waziri wa kazi, uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika Harouna Ali Suleiman amesema wafanyakazi wa vibarua kwa siku watalipwa shilingi elfu 10 kutoka shilingi 4,500 ya malipo ya zamani.

        Aidha amesema wafanyakazi wasiokuwa na ujuzi watalipwa shilingi elfu saba kwa siku kutoka shilingi 3,500 na wafanyakazi wa mjumbani watalipwa shilingi elfu 60 kutoka shilingi elfu 30 kwa mwezi sawa na ongezeko la asilimia 100.

        Waziri Suleiman amesema mishahara hiyo mipya itaanza kulipwa kuanzia tarehe mosi mwezi ujao na kuwataka wajiri kutekeleza agizo hilo la serikali la kuanza kulipa mishahara mipya.

        Hata hivyo amesema wajiri wanaweza kuowaongezea mishahara wafanyakazi wao kulingana na hali ya uzalishaji itakavyoruhusu kwenye sekta zao.

Kuhusu suala la mikataba kwa wafanyakazi wa sekta binafsi hasa kazi za majumbani amewataka wananchi wasikubali kufanya kazi kabla ya kufunga mktaba.

Mara ya mwisho serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ilipandisha mishahara ya watumishi wa sekta binafsi kwa shilingi elfu 70 kima cha chini mwaka 2008.

Advertisements