Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa

Serikali ya mapinduzi Zanziba imeombwa kuiandikia serikali ya jamhuri ya muungano Tanzania kuitaka kusimamisha mpango wa maombi ya kuongezewa eneo la ukanda wa bahari kuu katika umoja wa mataifa. Ombi hilo limetolewa na mwakilishi wa jimbo la Mji mkongwe Ismail Jussa alipowasilisha hoja ya dharura kuhusiana na hatua ya serikali ya Tanzania kuwasilisha ombi umoja wa mataifa kutaka kuongezewa maili 200 za ziada katika eneo la bahari kuu ya hindi. Amesema suala hilo bado halijapatiwa ufumbuzi kwa vile Zanzibar kupitia baraza la wawakilishi imetoa mapendekezo kwa serikali kuwa shughuli za eneo la bahari liwe chini ya mamlaka ya Zanzibar. Jussa amesema iwapo serikali ya muungano haitachukua hatua ya kusimamisha mpango huo serikali ya mapinduzi ipeleke ujumbe wake na barua rasmi katika umoja wa mataifa kutaka kusimamishwa maombi hayo. Katika pendekezo hilo lililowasilishwa kwenye umoja wa mataifa tarehe 18 mwezi huu, Tanzania imeomba kuongezewa eneo la ziada la kilomita za mraba elfu 61 katika ukanda wa bahari kuu. Kwa mujibu wa mwakilishi Jussa sehemu kubwa ya eneo hilo iliyoombwa la bahari kuu liko upande wa mashariki mwa visiwa vya Unguja na Pemba.

Advertisements