Archive for February, 2012

JOY APINGA KUVULIWA UONGOZI WA NLD

Naibu katibu mkuu wa chama cha NLD Rashid Ahmmed Joy anaedaiwa kuvuliwa uongozi wa chama hicho amesema bado ni kiongozi halali wa chama hicho na kuwataka wafuasi wa chama kupuza madai hayo.

Akizungumza na Zenji Fm radio juu ya hatama yake hiyo amesema kikao pekee kinachoweza kumvua uongozi ni mkutano wa halamashauri kuu wa chama hicho na sio vikao vingine.

Amesema yeye amechaguliwa kihalali mwaka 2008 katika mkutano mko wa NLD uliofanyika mkoani Mtwara na kusema hatambui madai ya kuvuliwa uongozi yaliofanywa na watu wachache….

Aidha Joy amesema uongozi wa juu unamtambua bado ni naibu katibu mkuu wa NLD upande wa Zanzibar na kuwataka wafuasi wa chama hicho kuendelea kushikiana nae katika kuimarisha uhai wa chama.

Hivi karibuni baadhi ya viongozi wa NLD upande wa Zanzibar walitoa taarifa za kwa vyombo vya habari za kuvuliwa uongozi Joy kwa madai ya kutohimili utendaji wa chama kutokana na hali yake ya kiafya.

Hata hivyo viongozi hao wamesema Joy atabakia kama mshauri wa chama hicho.

Advertisements

SAIDIENI UJENZI WA MADARASA NA VYUO VYUO VYA QUR-ANI

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AKIKAGUA MOJA YA DARASA LILIOMO NDANI YA JENGO LA MADRASA YA HIDAYATUL ISLAMIA YENYE WANAFUNZI 500 ILIYOPO NJIA KUU MOGA KATIKA WADI WA GAMBA WILAYA YA KASKAZINI A.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema ipo haja kwa Washirika na Wafadhili wa Maendeleo katika nyanja za Elimu ya Dini ndani na nje ya Nchi kufikiria zaidi wazo la  kuongeza nguvu katika ujenzi wa Vyuo na Madrasa ili kuwajengea mazingira bora ya Kitaaluma Watoto wa Taifa hili.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kulifunguwa Jengo Jipya la Madrasa Hidayatul Islamia iliyopo Njia Kuu Moga ndani ya Wadi ya Gamba Wilaya ya Kaskazini A.

Balozi Seif alisema Jamii ya Kiislamu imeshuhudia ongezeko kubwa la Ujenzi wa Misikiti Nchini kasi ambayo inaweza pia kuelekezwa katika Vyuo na Madrasa ambayo Maeneo mengi yamekuwa na ufinyu wa Majengo hao ya Kudumu.

“ Sisemi kwamba Wafadhili wasijenge Misikiti la hasha. Lakini ni vyema  kwa wafadhili wakaangalia mazingira ya Vyuo na Madrasa nyingi Nchini    ambazo ama ni mbovu au hazina hadhi ya kusomeshea kitabu cha Mwenyezi Muungu ”. Alishauri na Kusisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais waZanzibaralimpongeza Mfadhili wa Madrasda hiyo Ukti Asia Mohd waOmankwa juhudi zake za kusaidia kupanua Elimu ya Dini Hapa Nchini.

“ Nimevutiwa na Madrasa hii. Nilipoikagua ndani nimeona  Darasa la Watu Wazima. Hii ni ishara na fursa nzuri kwa nao kupata wasaa wa kujielimisha. Kwa kweli Madrasa zina umuhimu wa kipekee katika kutanua Elimu popote pale ”. Alifafanua Balozi Seif.

Balozi Seif aliwataka Vijana kuhakikisha wanaitafuta Elimu kwa Njia yoyote huku akiisisitiza Jumuiya inayosimamia masuala ya Elimu ya Dini Wilaya ya Kaskazini “A” { JUVMAWA } ikaendelea kuonyesha Njia bora kwa Watoto wanaowalea.         

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameahidi kutoa Mchango wa Kompyuta moja kwa ajili ya Madrasa hiyo na kuutaka Uongozi wa Jimbo la Chaani, Wilaya ya Kaskazini A na Mkoa wa Kaskazini kuhakikisha changamoto zinazoikabili Madrasa hiyo zinatatuliwa.

Katika Risala ya Madrasa hiyo iliyosomwa na Ustadhi Khamis Hakim alisema Madrasa hiyo iliyoasisiwa zaidi ya  miaka 80 ikiwa na Wanafunzi 500 mchanganyiko   imekuwa  chemchem ya kutoa walimu wanaoendelea kusomesha Madrasa tofauti Wilayani humo.

Wakati huo huo mamia ya Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi wamehudhuria Maulidi ya Uzawa wa  Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Mtume Muhammad { SAW }.

Maulidi hayo yaliandaliwa na Uongozi wa Masjid Noor Muhammad

{ SAW } iliyopo Mtaa waMombasakwaChinaambapo Makamu wa Pili wa Rais waZanzibarBalozi Seif alikuwa  Mgeni Rasmi kwenye Hafla hiyo.

Akitoa chakula cha moyo katika hadhara hiyo Mwanachuoni Maarufu ndani ya  Mwambao waTanzaniaSheikh Sameer Zulfikar  amewaasa Waumini wa Dini ya Kiislamu kutouacha Mwezi huu ukapita bila ya kusafisa nyoyo zao kwa kumtukuza Mtume Muhammad { SAW }.

 

WATU WENYE ULEMAVU PEMBA WAOMBA MSAADA WA KIMAISHA

Kampuni ya Zantel ikikabidhi msaada kwa watu wenye ulemavu ambao pia unahitajika kwa watu wenye ulemavu kisiwani Pemba

 

Watu wenye ulemavu katika shehia ya Ndagoni Pemba wameiomba serikali kuwasaidia kutokana na uwezo wao mdogo wa kiuchumi kuendesha familia zao.

        Wakizungumza na Zenji Fm radio, huko kijijini kwao Ndagoni watu hao wenye ulemavu wa aina tofauti wamesema baadhi ya walemavu katika kijiji hicho wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi kutokana na ulemavu wao, hivyo wameiomba serikali kuwasaidia.

        Mmoja wa watu wenye ulemavu Mohamme Said Hamad amesema anahitaji msaada wa baskeli na fedha za kufanya miradi ya ya kundeshea maisha yake, huku watu wengine wenye ulemavu wakiomba msaada kama huo….

        Nae sheha wa shehia ya Ndagoni Masoud Ali Mohammed akizungumza na mwandishi wetu juu ya maendeleo ya watu hao amesema wanahitaji misaada mbali mbali ya maendeleo ili kujikimu kimaisha.

        Aidha sheha huyo amependekeza kuwepo kwa kamati ya watu wenye ulemavu kijijini hapo ili kuhakikisha misaada yote inayotolewa kwa watu hao inawafika)

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR KUOMBA MSAADA KWA WASAMARIA WEMA

Waziri wa afya Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari

Wizara ya afya Zanzibar imewaomba watu wenye uwezo kusaidia matibabu ya watoto zaidi ya 100 wanaotaka kusafirishwa nje ya nchi kutokana na serikali kukabiliwa na ongezeko kubwa la wagonjwa hao.

Waziri wa wizara hiyo Juma Duni Haji amesema gharama za kuwasafirisha watoto hao ni kubwa na serikali haina uwezo wa kuwatosha kuwasafirisha watoto hao wanaougua maradhi ya figo, moyo na saratani.

Akizungumza na wandishi wa habari juu ya utekelezaji wa majukumu ya wizara katika kipindi cha miezi sita amesema kuanzia Julai 2011 hadi Desemba mwaka jana serikali imetumia zaidi ya shilingi milioni 255 kuwasafirisha wagonjwa nje ya nchi.

Hata hivyo amesema idadi ya wagonjwa ya watoto na watu wazima wanaohitaji kusafirishwa nje ya nchi inazidi kuongezeka, hivyo ni vyema  kwa watu wenye uwezo kusaidia juhudi za kuokoa maisha ya watu hao

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikipeleka wagonjwa wanaoshindikana kutibiwa katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja katika nchi za India na Israeli. 

Akizungumzia ujenzi wa chumba cha wagonjwa mahuti katika hospitali ya Mnazi mmoja Duni amesema wizara inaendelea na matengenezo ya chumba na serikali  imetoa shilingi milioni 500 kati ya milioni 900.

Amesema matengenezo hayo yanendelea vizuri na yanatarajiwa kukamilika kabla ya bajeti ya mwakani.

Kuhusu upungufu wa madaktari bingwa amesema madaktari waliopo 20 wanasaidiana na madaktari kutoka nchi za Cuba, Norway, Misri na China.

Amesema katika kukabiliana na hali hiyo serikali inawapa mafunzo zaidi ya vijana 30 chini ya usimamizi wa madaktari bingwa wa Cuba pamoja na kuingia mkataba na Norway kuleta madaktari bingwa na kupeleka madaktari wazalendo nchini humo kupata uzowefu.

MOHAMMED RAZA ASHINDA KWA KISHINDO

Mohammed Raza

Mgombea wa chama cha mapinduzi CCM Mohammed Raza ameshinda uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Uzini kwa kupata zaidi ya asilimia 90 ya kura. Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa tume ya uchaguzi Zanzibar, wilaya ya kati Mussa Ali Juma amesema Raza amepata kura elfu tano, 377 akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA Ali Mbarouk Mshimba kura 281. Mgombea wa CUF Salma Hussein Zaral amepata kura 223, mgombea wa TADEA Khamis Khatib Vuai kura 14 na mgombea wa AFP Rashid Yussuf Mchenga kura nane. Juma amesema watu waliojiandikisha katika uchaguzi huo ni elfu nane, 743, waliopiga kura elfu elfu tano, 903 na kura zilizoharibika 28. Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kutangazwa mwakilishi mteule Raza amesema kazi kubwa iliyoko mbele yake ni kupeleka maendeleo kwa wananchi wote wa jimbo la Uzini. Amesema kura alizopata sio za wana CCM pekee bali ni kura za wananchi wote wa jimbo la Uzini……

) Uchaguzi mdogo wa jimbo la Uzini umefanyika kufuatia kifo cha aliekuwa mwakilishi wa jimbo hilo kutoka CCM Marehemu Mussa Khamis Silima.

MELI YA MIZIGO YAWAKA MOTO ZANZIBAR

Meli ya mizigo iitwayo Yaarazak imeripuka leo jioni karibu na bandari ya Malindi Zanzibar

Meli moja ya mizigo Mv Jazak imeungua moto nangani nje ya bandari ya Malindi jana jioni.

Mwandishi wetu alieshuhudia tukio hilo amesema meli hiyo ilivutwa na meli nyingine kutoka eneo hilo na kupelekwa sehemu ya mbali ili kuepusha madhara zaidi karibu na eneo la bandari.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wameshangazwa kutokana na kutochukuliwa hatua yoyote ya kuzima moto uliokuwa ndani ya meli hiyo kwa haraka……

Hata hivyo hakuna mabaharia waliojeruhiwa wakati meli hiyo ilipokuwa ikiwaka moto na chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Akizungumza na zenji fm radio naibu waziri wa miundo mbinu na mawasiliano Issa Gavu  amesema meli hiyo kwa kipindi cha miezi minne iko nangani na ilikuwa inafanyiwa matengenezo.

Gavu amesema serikali bado inakabiliwa na tatizo la vifaa vya ukozi na kuzima moto

Meli hiyo iliyosajiliwa Zanzibar inamilikiwa na kampuni ya In Island Interprise ya Zanzibar.

Hii ni mara ya pili kwa meli zinalizokuwa nangani katika bandari ya Malindi kuwaka moto kufuatia meli ya Mv. Serengeti iliyoungua moto mwaka 2010.

MATOKEO YA KIDATU CHA PILI ZANIZIBAR 2011/2012

Form II Results 2011/2012 – Unguja

Form II Results 2011/2012 – Pemba