Serikali ya Iran imeipatia serikali ya Mapinduzi Zanzibar msaada wa matrekta madogo 50 yatakayotumika kwa kazi za kilimo cha umwagiliaji, maji. Msaada huo una lengo la kuendeleza sera ya mkakati wa mpango mpya wa kilimo cha mpunga , umegharimu zaidi ya dola laki mbili za Kimarekani. Akipokea msaada huo Kaimu Waziri wa Kilimo na Mali asili Ramadhan Abdulla Shaaban, amesema utasaidia Zanzibar katika kufanikisha sera ya kuimarisha kilimo cha kisasa cha umwagiliaji maji. Aidha amesema msaada huo utaiwezeshja Zanzibar kufikia lengo la uzalishaji wa zao la mpunga na kupunhuza uagiziaji wa mchele kutoka nje

 Nae balozi wa Iran nchini Tanzania Muhsin Mohavedin Gomi, amesema serikali ya nchi yake imetoa msaada huo kama ishara ya uhusiano nzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili. Amesema wakulima wa Zanzibar wanahitaji kusaidiwa kimataifa katika kutekeleza ya sera ya kuleta mabadiliko ya kilimo ili wajitosheleze kwa chakula. Msaada huo wa matrekta hayo umekabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika katika kiwanda cha Matrekta Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Advertisements