Meli ya mizigo iitwayo Yaarazak imeripuka leo jioni karibu na bandari ya Malindi Zanzibar

Meli moja ya mizigo Mv Jazak imeungua moto nangani nje ya bandari ya Malindi jana jioni.

Mwandishi wetu alieshuhudia tukio hilo amesema meli hiyo ilivutwa na meli nyingine kutoka eneo hilo na kupelekwa sehemu ya mbali ili kuepusha madhara zaidi karibu na eneo la bandari.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wameshangazwa kutokana na kutochukuliwa hatua yoyote ya kuzima moto uliokuwa ndani ya meli hiyo kwa haraka……

Hata hivyo hakuna mabaharia waliojeruhiwa wakati meli hiyo ilipokuwa ikiwaka moto na chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Akizungumza na zenji fm radio naibu waziri wa miundo mbinu na mawasiliano Issa Gavu  amesema meli hiyo kwa kipindi cha miezi minne iko nangani na ilikuwa inafanyiwa matengenezo.

Gavu amesema serikali bado inakabiliwa na tatizo la vifaa vya ukozi na kuzima moto

Meli hiyo iliyosajiliwa Zanzibar inamilikiwa na kampuni ya In Island Interprise ya Zanzibar.

Hii ni mara ya pili kwa meli zinalizokuwa nangani katika bandari ya Malindi kuwaka moto kufuatia meli ya Mv. Serengeti iliyoungua moto mwaka 2010.

Advertisements