Mohammed Raza

Mgombea wa chama cha mapinduzi CCM Mohammed Raza ameshinda uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Uzini kwa kupata zaidi ya asilimia 90 ya kura. Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa tume ya uchaguzi Zanzibar, wilaya ya kati Mussa Ali Juma amesema Raza amepata kura elfu tano, 377 akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA Ali Mbarouk Mshimba kura 281. Mgombea wa CUF Salma Hussein Zaral amepata kura 223, mgombea wa TADEA Khamis Khatib Vuai kura 14 na mgombea wa AFP Rashid Yussuf Mchenga kura nane. Juma amesema watu waliojiandikisha katika uchaguzi huo ni elfu nane, 743, waliopiga kura elfu elfu tano, 903 na kura zilizoharibika 28. Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kutangazwa mwakilishi mteule Raza amesema kazi kubwa iliyoko mbele yake ni kupeleka maendeleo kwa wananchi wote wa jimbo la Uzini. Amesema kura alizopata sio za wana CCM pekee bali ni kura za wananchi wote wa jimbo la Uzini……

) Uchaguzi mdogo wa jimbo la Uzini umefanyika kufuatia kifo cha aliekuwa mwakilishi wa jimbo hilo kutoka CCM Marehemu Mussa Khamis Silima.

Advertisements