Kampuni ya Zantel ikikabidhi msaada kwa watu wenye ulemavu ambao pia unahitajika kwa watu wenye ulemavu kisiwani Pemba

 

Watu wenye ulemavu katika shehia ya Ndagoni Pemba wameiomba serikali kuwasaidia kutokana na uwezo wao mdogo wa kiuchumi kuendesha familia zao.

        Wakizungumza na Zenji Fm radio, huko kijijini kwao Ndagoni watu hao wenye ulemavu wa aina tofauti wamesema baadhi ya walemavu katika kijiji hicho wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi kutokana na ulemavu wao, hivyo wameiomba serikali kuwasaidia.

        Mmoja wa watu wenye ulemavu Mohamme Said Hamad amesema anahitaji msaada wa baskeli na fedha za kufanya miradi ya ya kundeshea maisha yake, huku watu wengine wenye ulemavu wakiomba msaada kama huo….

        Nae sheha wa shehia ya Ndagoni Masoud Ali Mohammed akizungumza na mwandishi wetu juu ya maendeleo ya watu hao amesema wanahitaji misaada mbali mbali ya maendeleo ili kujikimu kimaisha.

        Aidha sheha huyo amependekeza kuwepo kwa kamati ya watu wenye ulemavu kijijini hapo ili kuhakikisha misaada yote inayotolewa kwa watu hao inawafika)

Advertisements