Naibu katibu mkuu wa chama cha NLD Rashid Ahmmed Joy anaedaiwa kuvuliwa uongozi wa chama hicho amesema bado ni kiongozi halali wa chama hicho na kuwataka wafuasi wa chama kupuza madai hayo.

Akizungumza na Zenji Fm radio juu ya hatama yake hiyo amesema kikao pekee kinachoweza kumvua uongozi ni mkutano wa halamashauri kuu wa chama hicho na sio vikao vingine.

Amesema yeye amechaguliwa kihalali mwaka 2008 katika mkutano mko wa NLD uliofanyika mkoani Mtwara na kusema hatambui madai ya kuvuliwa uongozi yaliofanywa na watu wachache….

Aidha Joy amesema uongozi wa juu unamtambua bado ni naibu katibu mkuu wa NLD upande wa Zanzibar na kuwataka wafuasi wa chama hicho kuendelea kushikiana nae katika kuimarisha uhai wa chama.

Hivi karibuni baadhi ya viongozi wa NLD upande wa Zanzibar walitoa taarifa za kwa vyombo vya habari za kuvuliwa uongozi Joy kwa madai ya kutohimili utendaji wa chama kutokana na hali yake ya kiafya.

Hata hivyo viongozi hao wamesema Joy atabakia kama mshauri wa chama hicho.

Advertisements