Archive for April, 2012

KAMATI KUU CCM YARIDHIA KUBADILISHWA BARAZA LA MAWAZIRI LA MUUNGANO

Wajumbe wa kamati kuu ya CCM

Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi CCM imeridhia uwamuzi wa rais Jakaya Kikwete wa kulifanyia mabadiliko baraza la mawaziri kufuatia ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali kutaja baadhi ya mawaziri kuhusika na ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka.
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nawiye amesema baadhi ya mawaziri na watendaji wa taasisi za serikali watawajibishwa kutokana na kuhusishwa na ubadhirifu wa mali za umma katika ripoti za mkaguzi mkuu wa serikali, kamati za bunge na mijadala ya bunge ya mkutano saba uliomalizika Jumatatu iliyopita……CLIPS…..(SAVED-NAPE)
Uwamuzi huo wa kamati kuu ya CCM umefikiwa katika kikao chake kinachofanyika mjini Dar es Salaam cha kupokea kupokea na kujadili taarifa za maazimio ya kamati ya wabunge wa CCM

BOTI YA SEA EXPRESS YANUSURIKA KUZAMA IKIWA NA ZAIDI YA ABIRIA 120

Boti ya Sea Express

WATU MIA MOJA NA ISHIRINI NA NNE WAMENUSURIKA KUFA MAJI BAADA YA BOTI  YA SEA EXPRESS  WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA PEMBA KUELEKEA UNGUJA KUPATA HITILAFU KATIKA INJINI  YAKE  KUTOKA MAILI SABA BANDARI YA PEMBA.

KWA MUJIBU WA KEPTAINI MKUU WA SHIRIKA LA BADANDARI BW. MAKAME HASSAN AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO AMBAPO AMEFAHAMISHA KUWA BOTI HIYO ILIYOKUWA NA ABIRIA MIA MOJA NNE NA WATOTO KUMI NA MBILI NA WAFANYAKAZI WANANE ILIPATA HITILAFU HIYO KUTOKA BANDARI YA MKOANI NA KUWAFANYA WATU KUWA NA WAKATI MGUMU.

AKITHIBITISHA TUKIO HILO KEPTENI WA MELI HIYO BW USSI ALI USSI AMESEMA WAMEPATA HITILAFU KATIKA INJINI KUTOKANA NA MASHINE YA KUCHUJIA MAFUTA (FILTER) KUSHINDWA KUFANYAKAZI KIKAMILIFU  NA UWEZO WA KUTEMBEA KATIKA KIWANGO CHA KAWAIDA ULIPUNGUA KUFUATIA   MAFUTA KUTOKUCHANGANYA VIZURI KWENYE INJINI.

 AMESEMA BAADA YA KUTOKEA HITALAFU HIYO ALIFANYA MAWASILIANO NA BANDARI YA MKOANI NA BANDARI YA UNGUJA BILA YA MAFANIKIO KUTOKANA NA UMBALI ULIOKUWEPO NA ALIMPIGIA WAKALA WAKE WA MELI PEMBA KUMJULISHA HALI HIYO ILI AWEZE KUCHUKUA HATUA ZA KUTAFUTA CHOMBO CHA KUSAIDIA.

AMEELEZA KWAMBA MIONGONI MWA VYOMBO VILIVYOOMBWA KUTOA MSAADA BAADA YA MAWASILIANO NI BOTI ZA KMKM, JITIHADA NA SERENGETI, LAKINI BOTI HIYO ILITENGENEA NA KUANZA SAFARI YAKE.

NAE FUNDI MKUU WA BOTI HIYO BW RICHARD SAMUEL AMESEMA KUWA BAADA YA KUTOKEA HITILAFU YA KIUFUNDI ALICHUKUA JUHUDI YA KUFANYIA MATENGENEZO KWA KUPITISHA MPIRA KUTOKA KATIKA CHUJIO NA KUPITISHA KWENYE TANGI LA MAFUTA MOJA KWA MOJA NA KUFANIKIWA KUFIKA SALAMA BANDARINI.

SHIRIKA LA UTANGAZAJI LIMEZUNGUMZA NA BAADHI ABIRIA WALIOKUWAMO KATIKA CHOMBO HICHO  NA WAMETHIBISHA KUTOKEA KWA HITILAFU HIZO ZILIZOCHUKUWA MUDA MREFU NA KUWAFANYA KUWA NA KUTAHARUKI

KIU YA WATANZANIA KUTAKA KUSIKIA KAULI YA PINDA KUWAJIBISHA MAWAZIRI YAISHA PATUPU

Waziri mkuu Mizengo Peter Pinda

Kiu ya watanzania ya kutaka kusikia tamko la serikali ya jamhuri ya muungano Tanzania juu ya madai ya wabunge kutaka kuwajibisha baadhi ya mawaziri wanaodaiwa kufanya ubadhirifu imeishia bila ya mafanikio.

        Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya wabunge kutishia kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na serikali yake.

Waziri mkuu Mizengo Pinda ambae alitarajiwa kutoa tamko hilo hakuelezea lolote juu ya madai hayo wakati wa kuakhirisha kikao cha bunge na badala yake aligusia mambo mengine ikiwemo mabadiliko ya katiba.

Pinda amesema mabadiliko ya kikatiba yanayotaka kufanyika nchini hayana lengo la kuwepo au kutokuwepo kwa jamhuri ya muungano Tanzania, hivyo amewataka viongozi kuwaelimisha wananchi juu ya mambo ya msingi wakati wa kutoa maoni ya undwaji wa katiba hiyo.

Hata hivyo Pinda amesema bado taifa linakabiliwa na changamoto kadhaa, hivyo kila mmoja anawajibu wa kutekeleza wajibu wake katika kufikia maendeleo ya nchi

Mbunge wa CHADEMA John Mnyika akizungumzia hoja hiyo ya kutaka kumpigia kura waziri mkuu kutokuwa na imani naye, amesema wametimiza masharti juu ya hoja hiyo kwa kusiniwa na wabunge 74.

Amesema hoja hiyo imewasilishwa kabla ya waziri mkuu kuhitimisha mkutano wa saba wa bunge na iwapo matarajio yao hayatafikiwa watarudi kwa wananchi kutaka uwajibikaji wa haraka

WAKATI HUO HUO

Spika wa bunge Anna Makinda amewataka mawaziri na wabunge kujieepusha na mambo ya chuki, uhasama na uadui kufuatia shutuma kali zilizotolewa kwa baadhi ya mawaziri katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza mara baada ya kuakhirishwa kikao cha mkutano wa saba wa bunge amesema yaliojadiliwa ndani ya kikao hicho ni kwa ajili ya nia njema badala ya kubeba chuki na kuwataka viongozi hao kuendelea na urafiki wao.

Amesema mawaziri waliosemwa vibaya ndio majukumu yao kwa vile vyeo ni dhamana hivyo si vyema kuchukua tuhuma hizo kwa hasira lakini walikumbushwa utekelezaji wa majukumu yao

Aidha Makinda amewataka wabunge kusoma zaidi kanuni zinazoendesha bunge hilo kutokana na yale wanayosema yako wazi, lakini bunge hilo linaendeshwa kwa taratibu maalum.

WANAHARAKATI12 WA ZANZIBAR WANAOPINGA MUUNGANO WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Wanaharakati 12 wanaodai uhalali wa kuwepo kwa Muungano TanganyikaZanzibarwamepandishwa katika mahaka ya Wilaya mwanakwerekwe wakikabiliwa na tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali na kusimama inje ya baraza wawakilishi wakiwa na mabango ya  kuukataaa Muungano.
.
Wanaharakati hao wamefikishwa katika mahakama hiyo ya wilaya iliyo chini ya hakimu Omar Mcha Hamza na kusomewa mashitaka matatu tofauti ambayo hata hivyo waliyakana.
Waliofikishwa mahakamani hapo ni Rashid Salum Ali (48) mkaazi wa Kikwajuni, Khamis Hassan Hamadi (51) wa Jang’ombe, Rashid Ali Rashid (21) anayeishi Mombasa, Hashim Juma Issa (54) mkaazi wa Mbweni, Suleiman Mustafa Suleiman (31) wa Mombasa pamoja na Haji Sheha Hamadi (49) anayeishi Chumbuni.
Wengine ni Rami Mbaraka Ahmed (48) wa Michenzani, Salum Massoud Juma (38) anayeishi Rahaleo, Mussa Omar Kombo (67) mkaazi wa Mpendae, Omar Kombo Is-hak (21) wa Magogoni, Ali Omar Omar (54) anayeishi Bububu na Massoud Faki Massoud (31) mkaazi wa Kilimahewa.
Wote hao kwa pamoja wameshitakiwa kwa makosa ya kufanya mkusanyiko usio halali, kuendelea kukusanyika baada ya kutangazwa kutawanyika na Ofisa wa Pilisi pamoja na shitaka la uhuni na uzururaji.
Mashitaka hayo yaliwasilishwa na Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo Said Ahmed Mohammed, Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Awali akiwa mahakamani hapo, Mwanasheria huyo wa serikali aliwasomea watuhumiwa hao shitaka la kufanya mkusanyiko usio halali kinyume na vifungu vya 55 (1) (2) (3) na 56 vya kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Katika shitaka hilo aliifahamisha mahakama kwa kudai kuwa, April 20 mwaka huu, majira ya saa 2:30 za asubuhi, huko Mbweni wilaya ya Magharibi Unguja, kwa pamoja na bila ya halali walijikusanya katika barabara ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Alidai kuwa, mkusanyiko huo uliwafanya majirani na watu waliokuwa wanakwenda kwenye Baraza kupata khofu, kuwa wangeliweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati hawakuwa na sababu za msingi za kukusanyika.
Kuhusu shitaka la kuendelea kukusanyika baada ya kutangazwa kutawanyika na Ofisa wa Polisi, Mwanasheria huyo alidai kuwa baada ya mkusanyiko huo walitakiwa kutawanyika kwa amani na Ofisa wa Polisi, lakini waliendelea kukusanyika kinyume cha sheria.
Kwa mujibu wa Mwanasheria huyo, kitendo hicho cha kukataa amri hiyo halali ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 60 cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Shitaka la mwisho linalowakabili watuhumiwa hao ni la uhuni na uzururaji, ambapo mahakama ilifahamishwa kuwa siku hiyo walipatikana wakiwa wamejikusanya kwenye barabara hiyo ya Baraza la Wawakilishi, wakiwa na mabango yenye maneno yanayopinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kitendo hicho ambacho ni kosa chini ya kifungu cha 182 (d) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar, ambacho walidaiwa kukifanya katika wakati na mazingira yanayoonesha kuwa hawakuwa na madhumuni halali.
Mahakama ilipowapa nafasi watuhumiwa hao kujibu madai hayo ya upande wa mashitaka waliyakana, na Mwanasheria huyo wa serikali kudai kuwa upelelezi wake bado haujakamilika.
Hivyo aliiomba mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa, ili kutoa nafasi ya kuweza kukamilisha upelelezi huo.
Baada ya hoja hizo, watuhumiwa hao waliomba mahakama hiyo iwapatie dhamana ombi ambalo hata hivyo upande huo wa mashitaka haukuwa na pingamizi nalo, iwapo watakuwa na wadhamini madhubuti watakaoweza kutekeleza masharti ya dhamana yatakayotolewa na mahakama.
Kwa kuzingatia hoja za pande mbili hizo, hakimu Omar Mcha Hamza pamoja na kuwapatia watuhumiwa hao masharti ya dhamana lakini alifahamisha kuwa endapo watashindwa kuyatekeleza watalazimika kubakia rumande.
Masharti hayo kila mtuhumiwa, awasilishe dhamana ya fedha taslimu shilingi 500,000 pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho kikiwemo cha Mzanzibari Mkaazi, na mmoja kati ya wadhamini hao awe ni mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Aidha hakimu huyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Mei 7 mwaka huu kwa kutajwa, na hadi mwandishi wa habari hizi anaondoka mahakamani hapo, ndugu na jamaa wa watuhumiwa hao walikuwa katika harakati za kuwadhamini.

SMZ KUPIGA MARUFUKU MAKONGAMANO NA MIHADHARA INAYOCHAFUA AMANI

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema haitakivumilia kikundi chochote kitakachoendesha makongamano na mihadhara itakayonekana kuhatarisha amani, utulivu na umoja wa wananchi.
Akiakhirisha kikao cha baraza la wawakilishi makamo wa pili wa rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amesema kumejitokeza kikundi cha wachache kinachoendesha makongamano na mihadhara inayotishia amani na utulivu.
Amesema makongamano na mihadhara inayoendeshwa na vikundi hivyo imebadili sura na kuwa kashfa, kejeli na matusi ya nguoni dhidi ya viongozi na wale wanaunga mkono muungano jambo ambalo ni kinyume na utamaduni wa mzanzibari na misingi ya demokrasia

Hata hivyo Balozi Iddi amewataka watanzania kuitumia fursa iliyotolewa na serikali ya kuandaa katiba mpya inayonesha kukuwa kwa demokrasia badala ya baadhi ya watu kujitokeza kuharibu dhamira hiyo.
Kuhusu taarifa ya kamati teuli iliyowasilishwa katika baraza la wawakilishi balozi Iddi amesema taarifa hiyo itasaidia kuwabadilisha viongozi wandamizi wa serikali kwa kufanya kazi kwa kujituma badala ya kimazowea.
Amesema rais Shein ametoa nafasi kwa kiongozi asietaka kubadilika kumuona kwa ajili ya kumpumzisha, hivyo amewataka mawaziri kusimamia kazi zao kwa uadilifu na uwajibikaji

Kikao cha baraza la wawakilishi kimeghirishwa hadi june 13 mwaka huu.

MWAKANJUKI AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali mstaafu Adam Clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam leo.
Marehemu Mwakanjuki amefariki duani mchana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani, lakini alilipata ulemavu uliotokana na ajali ya gari wakati akierejea mjini Dodoma katika mkoa wa Morogoro miaka minne iliyopita.
Tokea kupaAliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali mstaafu Adam Clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam leo.
Marehemu Mwakanjuki amefariki duani mchana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani, lakini alilipata ulemavu uliotokana na ajali ya gari wakati akierejea mjini Dodoma katika mkoa wa Morogoro miaka minne iliyopita.
Tokea kupata ajali hiyo mwaka 2007 marehemu Mwakanjuki hajawahi kuonekana hadharani kufuatia kupewa likizo ya maradhi wakati wa serikali ya awamu ya saba iliyongozwa na Dr. Amani Abeid Karume.
Akitoa taarifa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya kifo hicho spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho amesema matayarisho ya kusafirisha mwili wa marehemu yanafanywa…….Mwakanjuki ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe nchini alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa kilimo na mifugo, waziri wa nchi ofisi ya rais katiba na utawala bora, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za miko na vikosi vya SMZ, mjumbe wa baraza la wawakilishi na waziri wa mawasiliano na uchukuzi.
Mwakanjuki pia alikuwa afisa mwandamizi katika jeshi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali na ameongoza brigedi mbali mbali ikiwemo jeshi la kujenga taifa JKT.
Hadi kufikia mwaka 2010 Marehemu alikuwa waziri wa mawasiliano a uchukuzi Zanzibar pamoja na kuwa mjumbe wa NEC hadi mauti yanamkuta.
ta ajali hiyo mwaka 2007 marehemu Mwakanjuki hajawahi kuonekana hadharani kufuatia kupewa likizo ya maradhi wakati wa serikali ya awamu ya saba iliyongozwa na Dr. Amani Abeid Karume.
Akitoa taarifa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya kifo hicho spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho amesema matayarisho ya kusafirisha mwili wa marehemu yanafanywa
Mwakanjuki ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe nchini alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa kilimo na mifugo, waziri wa nchi ofisi ya rais katiba na utawala bora, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za miko na vikosi vya SMZ, mjumbe wa baraza la wawakilishi na waziri wa mawasiliano na uchukuzi.
Mwakanjuki pia alikuwa afisa mwandamizi katika jeshi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali na ameongoza brigedi mbali mbali ikiwemo jeshi la kujenga taifa JKT.
Hadi kufikia mwaka 2010 Marehemu alikuwa waziri wa mawasiliano a uchukuzi Zanzibar pamoja na kuwa mjumbe wa NEC hadi mauti yanamkuta.

WAVUVI WAWAJIA JUU WAWAKILISHI WANAOPINGA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA UVUVI

 

          Image  WENYEVITI WA KAMATI YA WAVUVI WA HIFADHI YA GHUBA YA MENAI WAMEWATAKA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WANAOPINGA UTEKELEZAJI WA SHERIA MPYA YA UVUVI KUWAOMBA RADHI.

KAULI HIYO YA WENYEVITI HAO IMEKUJA KUFUATIA KUWEPO NA KAULI ZA BAADHI YA WAJUMBE WA BARAZAHILOWAKIDAI SHERIA HIYO HAINA MASLAHI KWA WAVUVI.

WAKITOA TAMKO LA KUUNGA MKONO SHERIA HIYO, HUKO KIZIMKAZI WENYEVI HAO WAMEWATAKA WAWAKILISHIHAO KUONANA NA WAVUVI WENYEWE KUZUNGUMZIA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA SHERIA HIYO.

KATIBU WA KAMATI TENDAJI WA HIFADHI HIYO MOHAMMED SULEIMAN AMESEMA SHERIA HIYO MBALI YA KULINDA SEKTA YA UVUVI LAKINI PIA INAIMARISHA SEKTA YA UTALII NA AJIRA.

AMESEMA SHERIA HIYO IMEWASHIRIKISHA WAVUVI WENYEWE, LAKINI BAADHI YA VIONGOZI WANADAI HAINA MASLAHI KUTOKANA NA MIRADIYAOYA UVUVI KUBANWA NA UTEKELEZAJI WA SHERIA.

NAE MWENYEKITI WA KAMATI YA UVUVI YA KIGAENI MKUNDUCHI, ZAHOR HAMAD ISSA AMESEMA VYOMBO VINGI VYA UVUVI VINAVYODAIWA KUVUA UVUVI HARAMU NI VILE VYA WANASIASA.

HIVYO AMESEMA UTEKELEZAJI WA SHERIA HIYO UMEATHIRI MASLAHI YAO, LAKINI WAVUVI WENGI WAMEFAIDIKA KUFUATIA KUPUNGUA KWA MITEGO HARAMU YA UVUVI.

ENEO LA GHUBA YA HIFADHI YA MINAI ILIYOANZIA MAZIZINI WILAYA MJINI HADI KIJIJI CHA BWEJUU WILAYA YA KATI INAJUMUISHA VIVJIJI 30 VYENYE ZAIDI YA WAVUVI LEFUTISANA 500.

SHERIA HIYO ILIYOANZA KUTEKELEZWA HIVI KARIBUNI IMEZUSHA MIGONGANO BAINA YA WAVUVI NA SERIKALI INAPINGA KUTUMIA UVUVI WA BUNDUKI, NYAVU ZA KUKOKOTA, MABOMU, MTANDO NA UTUPA.