RAIS WAZANZIBARNA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DK ALI MUHAMMED SHEIN  LEO  AMEWABADILISHA BAADHI YA MAWAZIRI KATIKA  BAADHI YA WIZARA.

KWA MUJIBU WA TAARIFA  ILIYOTOLEWA NA KATIBU MKUU WA BARAZA LA MAPINDUZI  NA KATIBU MKUU KIONGOZI  DK. ABDULHAMID YAHYA MZEE  MAWAZIRI WALIOBADILISHWA WIZARA NI PAMOJA NA  MHE. RAMADHANI ABDALLA SHAABAN  AMBAYE SASA ANAKUWA WAZIRI WA  ARDHI, MAKAAZI  MAJI NA NISHATI NA MHE.  ALI JUMA SHAMUHUNA ANAKUWA WAZIRI WA ELIMU  NA MAFUNZO YA AMALI.

 KABLA YA MABADILIKO HAYO MHE. RAMADHANI ABDALLA SHAABAN ALIKUWA NI WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI WAKATI MHE. ALI JUMA SHAMUHUNA ALIKUWA WAZIRI WA  ARDHI MAKAAZI, MAJI NA NISHATI.

WENGINE WALIOBADILISHWA WIZARA NI MHE.  MANSOUR YUSSUF HIMID AMBAE SASA ANAKUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAPINDUZI NA WAZIRI ASIYEKUWA NA WIZARA MAALUM WAKATI MHE SULEIMAN OTHMAN  NYANGA ANAKUWA  WAZIRI WA KILIMO  NA MALIASILI.

KABLA YA MABADILIKO HAYO MHE,  MANSOUR ALIKUWA NI WAZIRI WA  KILIMO NAMALIASILI WAKATI MHE. SULEIMAN OTHMAN NYANGA ALIKUWA NI MJUMBE WA BARAZA LA MAPINDUZI NA WAZIRI ASIYEKUWA NA WIZARA MAALUM.

            TAARIFA HIYO YA KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI NA KATIBU MKUU KIONGOZI  PIA IMEELEZA KUWA  MHE. ABDILLAH  JIHAD HASSAN SASA ANAKUWA  WAZIRI WA  MIFUGO NA UVUVI WAKATI MHE.  SAIDI ALI MBAROUK AMETEULIWA KUWA  WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO.

KABLA YA MABADILIKO HAYO MHE.  ABDILLAH JIHAD HASSAN ALIKUWA NI WAZIRI  WA HABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO WAKATI MHE.  SAIDI ALI MBAROUK ALIKUWA NI WAZIRI WA MIFUGO NA  UVUVI.

AIDHA, RAIS WAZANZIBARNA MWENYEKLITI WA BARAZA LA MAPINDUZI  DKT ALI MUHAMMED SHEIN AMEMTEUA  BW. SHEHA MOHAMMED SHEHA KUWA  MSHAURI WA RAIS PEMBA.

Advertisements