UTURUKI IMEAHIDI KUENDELEZA UHUSIANO NA USHIRIKIANO KATI YAKE NA  ZANZIBAR KATIKA KUIMARISHA SEKTA ZA MAENDELEO IKIWEMO ELIMU, KILIMO, AFYA NA UTALII.

            AKIZUNGUMZA NA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK ALI MOHAMMED SHEIN  BALOZI WA UTURUKI NCHINI TANZANIA  BW ALI DAVUTOGLU ALIEFIKA IKULU KUJITAMBULISHA AMESEMA NCHI  YAKE ITAHAKIKISHA MAKUBALIANO YALIOFIKIWA KATIKA KUIMARISHA SEKTA HIZO YANATEKELEZWA KWA UFANISI MKUBWA.

            KWA UPANDE WA SEKTA YA ELIMU AMESEMA KUMEKUWA NA USHIRIKIANO MZURI KATI YA NCHI HIYO NA ZANZIBAR  KUPITIA CHUO  KIKUU CHA TAIFA CHA SUZA AMBAPO WAMEANZISHA PROGRAMU MBALI MBALI ZA KITAALUMA PAMOJA NA KUKIIMARISHA CHUO HICHO KWA KUONGEZA NYENZO ZA MAFUNZO.

            AKIZUNGUMZIA SEKTA YA KILIMO AMESEMA ATAHAKIKISHA UTAALAMU WA UIMARISHAJI WA KILIMO ULIOFIKIWA NCHINI UTURUKI  PIA, UNAWAFIKIA WATAALAMU WA  ZANZIBAR KWA KUTOA MAFUNZO NA KUBADILISHANA UZOEFU KWA LENGO LA KUKUZA SEKTA HIYO NCHINI.            

 NAE DK. SHEIN AMETOA SHUKURANI KWA BALOZI HUYO PAMOJA NA NCHI YAKE  KUTOKANA NA AZMA YA  KUIUNGA MKONO ZANZIBAR KATIKA SEKTA ZA MAENDELEO HASA ELIMU, AFYA, KILIMO, UTALII NA NYENGINEZO.

            AMESEMA ZANZIBAR INATHAMINI UHUSIANO NA USHIRIKIANO MKUBWA ULIOPO KATI YAKE NA  NCHI HIYO NA KUSISITIZA KUWA UTAIMARISHWA NA KUENDELEZWA KWA MANUFAA YA PANDE ZOTE.

            DK. SHEI AMESEMA ANAMATUMAINI MAKUBWA YA KUFIKIA MALENGO YALIOKUSUDIWA KATIKA KUENDELEZA UHUSIANO HUO HASA KATIKA SEKTA HIZO ZA MAENDELEO AMBAPO MCHAKATO WAKE UMEANZA VIZURI.

 WAKATI HUO HUO, DK. SHEIN AMEFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA BURUNDI NCHINI TANZANIA  BWANA ISSA NTAMBUKA ALIYEKUJA KUJITAMBULISHA AMBAPO WALIELEZEA KUKUZA UHUSIANO NA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA ZA MAENDELEO HASA ELIMU.

            DK. SHEIN PIA, AMEZUNGUMZA NA BALOZI MPYA WA TANZANIANCHINI ITALIA, MHE. JAMES ALEX ALIYEFIKA IKULU KWA AJILI YA KUMUAGA.

Advertisements