Image  WENYEVITI WA KAMATI YA WAVUVI WA HIFADHI YA GHUBA YA MENAI WAMEWATAKA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WANAOPINGA UTEKELEZAJI WA SHERIA MPYA YA UVUVI KUWAOMBA RADHI.

KAULI HIYO YA WENYEVITI HAO IMEKUJA KUFUATIA KUWEPO NA KAULI ZA BAADHI YA WAJUMBE WA BARAZAHILOWAKIDAI SHERIA HIYO HAINA MASLAHI KWA WAVUVI.

WAKITOA TAMKO LA KUUNGA MKONO SHERIA HIYO, HUKO KIZIMKAZI WENYEVI HAO WAMEWATAKA WAWAKILISHIHAO KUONANA NA WAVUVI WENYEWE KUZUNGUMZIA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA SHERIA HIYO.

KATIBU WA KAMATI TENDAJI WA HIFADHI HIYO MOHAMMED SULEIMAN AMESEMA SHERIA HIYO MBALI YA KULINDA SEKTA YA UVUVI LAKINI PIA INAIMARISHA SEKTA YA UTALII NA AJIRA.

AMESEMA SHERIA HIYO IMEWASHIRIKISHA WAVUVI WENYEWE, LAKINI BAADHI YA VIONGOZI WANADAI HAINA MASLAHI KUTOKANA NA MIRADIYAOYA UVUVI KUBANWA NA UTEKELEZAJI WA SHERIA.

NAE MWENYEKITI WA KAMATI YA UVUVI YA KIGAENI MKUNDUCHI, ZAHOR HAMAD ISSA AMESEMA VYOMBO VINGI VYA UVUVI VINAVYODAIWA KUVUA UVUVI HARAMU NI VILE VYA WANASIASA.

HIVYO AMESEMA UTEKELEZAJI WA SHERIA HIYO UMEATHIRI MASLAHI YAO, LAKINI WAVUVI WENGI WAMEFAIDIKA KUFUATIA KUPUNGUA KWA MITEGO HARAMU YA UVUVI.

ENEO LA GHUBA YA HIFADHI YA MINAI ILIYOANZIA MAZIZINI WILAYA MJINI HADI KIJIJI CHA BWEJUU WILAYA YA KATI INAJUMUISHA VIVJIJI 30 VYENYE ZAIDI YA WAVUVI LEFUTISANA 500.

SHERIA HIYO ILIYOANZA KUTEKELEZWA HIVI KARIBUNI IMEZUSHA MIGONGANO BAINA YA WAVUVI NA SERIKALI INAPINGA KUTUMIA UVUVI WA BUNDUKI, NYAVU ZA KUKOKOTA, MABOMU, MTANDO NA UTUPA.

 

Advertisements