Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali mstaafu Adam Clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam leo.
Marehemu Mwakanjuki amefariki duani mchana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani, lakini alilipata ulemavu uliotokana na ajali ya gari wakati akierejea mjini Dodoma katika mkoa wa Morogoro miaka minne iliyopita.
Tokea kupaAliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali mstaafu Adam Clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam leo.
Marehemu Mwakanjuki amefariki duani mchana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani, lakini alilipata ulemavu uliotokana na ajali ya gari wakati akierejea mjini Dodoma katika mkoa wa Morogoro miaka minne iliyopita.
Tokea kupata ajali hiyo mwaka 2007 marehemu Mwakanjuki hajawahi kuonekana hadharani kufuatia kupewa likizo ya maradhi wakati wa serikali ya awamu ya saba iliyongozwa na Dr. Amani Abeid Karume.
Akitoa taarifa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya kifo hicho spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho amesema matayarisho ya kusafirisha mwili wa marehemu yanafanywa…….Mwakanjuki ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe nchini alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa kilimo na mifugo, waziri wa nchi ofisi ya rais katiba na utawala bora, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za miko na vikosi vya SMZ, mjumbe wa baraza la wawakilishi na waziri wa mawasiliano na uchukuzi.
Mwakanjuki pia alikuwa afisa mwandamizi katika jeshi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali na ameongoza brigedi mbali mbali ikiwemo jeshi la kujenga taifa JKT.
Hadi kufikia mwaka 2010 Marehemu alikuwa waziri wa mawasiliano a uchukuzi Zanzibar pamoja na kuwa mjumbe wa NEC hadi mauti yanamkuta.
ta ajali hiyo mwaka 2007 marehemu Mwakanjuki hajawahi kuonekana hadharani kufuatia kupewa likizo ya maradhi wakati wa serikali ya awamu ya saba iliyongozwa na Dr. Amani Abeid Karume.
Akitoa taarifa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya kifo hicho spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho amesema matayarisho ya kusafirisha mwili wa marehemu yanafanywa
Mwakanjuki ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe nchini alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Advertisements