Boti ya Sea Express

WATU MIA MOJA NA ISHIRINI NA NNE WAMENUSURIKA KUFA MAJI BAADA YA BOTI  YA SEA EXPRESS  WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA PEMBA KUELEKEA UNGUJA KUPATA HITILAFU KATIKA INJINI  YAKE  KUTOKA MAILI SABA BANDARI YA PEMBA.

KWA MUJIBU WA KEPTAINI MKUU WA SHIRIKA LA BADANDARI BW. MAKAME HASSAN AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO AMBAPO AMEFAHAMISHA KUWA BOTI HIYO ILIYOKUWA NA ABIRIA MIA MOJA NNE NA WATOTO KUMI NA MBILI NA WAFANYAKAZI WANANE ILIPATA HITILAFU HIYO KUTOKA BANDARI YA MKOANI NA KUWAFANYA WATU KUWA NA WAKATI MGUMU.

AKITHIBITISHA TUKIO HILO KEPTENI WA MELI HIYO BW USSI ALI USSI AMESEMA WAMEPATA HITILAFU KATIKA INJINI KUTOKANA NA MASHINE YA KUCHUJIA MAFUTA (FILTER) KUSHINDWA KUFANYAKAZI KIKAMILIFU  NA UWEZO WA KUTEMBEA KATIKA KIWANGO CHA KAWAIDA ULIPUNGUA KUFUATIA   MAFUTA KUTOKUCHANGANYA VIZURI KWENYE INJINI.

 AMESEMA BAADA YA KUTOKEA HITALAFU HIYO ALIFANYA MAWASILIANO NA BANDARI YA MKOANI NA BANDARI YA UNGUJA BILA YA MAFANIKIO KUTOKANA NA UMBALI ULIOKUWEPO NA ALIMPIGIA WAKALA WAKE WA MELI PEMBA KUMJULISHA HALI HIYO ILI AWEZE KUCHUKUA HATUA ZA KUTAFUTA CHOMBO CHA KUSAIDIA.

AMEELEZA KWAMBA MIONGONI MWA VYOMBO VILIVYOOMBWA KUTOA MSAADA BAADA YA MAWASILIANO NI BOTI ZA KMKM, JITIHADA NA SERENGETI, LAKINI BOTI HIYO ILITENGENEA NA KUANZA SAFARI YAKE.

NAE FUNDI MKUU WA BOTI HIYO BW RICHARD SAMUEL AMESEMA KUWA BAADA YA KUTOKEA HITILAFU YA KIUFUNDI ALICHUKUA JUHUDI YA KUFANYIA MATENGENEZO KWA KUPITISHA MPIRA KUTOKA KATIKA CHUJIO NA KUPITISHA KWENYE TANGI LA MAFUTA MOJA KWA MOJA NA KUFANIKIWA KUFIKA SALAMA BANDARINI.

SHIRIKA LA UTANGAZAJI LIMEZUNGUMZA NA BAADHI ABIRIA WALIOKUWAMO KATIKA CHOMBO HICHO  NA WAMETHIBISHA KUTOKEA KWA HITILAFU HIZO ZILIZOCHUKUWA MUDA MREFU NA KUWAFANYA KUWA NA KUTAHARUKI

Advertisements