—Sala ya pamoja iliyosaliwa leo katika viwanja Maisara iliyotayarishwa na Taasisi za Kiislamu Zanzibar

Taasisi za kislamu Zanzibar zimetishia kuwachukulia hatua za kisheria viongozi au taasisi za serikali zitakazojaribu kuzuwia mihadhara yao ya kuwaelimisha wananchi juu ya mabadiliko ya katiba mpya.

        Akizungumza katika ibada ya maalum huko viwanja vya Maisara amiri wa jumuiya ya maimam Farid Hadi amesema mihadhara wanayoitoa  inaendana sambamba na uhuru wa maoni na kuabudu kama ilivyo ainishwa katika katiba ya Zanzibar..

        Hivyo amesema hakuna taasisi yoyote itakayoweza kuwazuwia shughuli zao na iwapo kutajitokeza watu wachache kufanya hivyo watawapeleka mahakamani.

Sheikh Hadi amesema taasisi za kislamu zinaendesha mihadhara hiyo kwa amani na utulivu na kukanusha madai inachochea vurugu

Mhadhara huo uliombatana na dua maalum pia ulizungumzia matatizo ya muungano ikiwemo utozaji wa kodi kubwa inayosababisha hali ngumu ya maisha

Matamsihi hayo ya taasisi hizo yamekuja kufuatia taarifa ya serikali iliyotolewa hivi karibuni kutaka kuvipiga marufuku vikundi vya watu vinavyovunja sheria katika kuwaelimisha wananchi juu ya mabadiliko ya katiba.

Mwandishi wetu alietembelea maeneo ya manispaa ya mji wa Zanzibar amesema baadhi ya maduka ya Darajani yalifungwa kwa muda kutokana na watu kuhudhuria katika ibada hiyo

Advertisements