BOTI  ya seaguall ambayo imepata matatizo katika injia yake na kusababisha kupoteza muelekeo kwa saa kadhaa wakati ikitoka pemba kuelekelea unguja imewasili salama katika bandari ya zanzibar ikiwa na abiria wapatao 354.

kwa mujibu wa mhandisi mkuu wa meli hiyo ndugu. saidi yahya amesema kuwa meli hiyo il.ianza kupata matatizo katika injiNI ZAKE NA KUZIMIKA HALI ILIYOSABABISHA KUSUKUMWA NA MAWIMBI MAKUBWA HADI KUPOTEZA MUELEKEO.

 MHANDISI HUYO AMESEMA KUWA KWA MUDA WA SAA TATU MELI ILIKUWA IKIPIGWA MAWIMBI NA KUPOTEZA MUELEKEO KUELEKEA NJE YA BANDARI YA PEMBA AMBAPO MATATIZO HAYO YALITOKEA KATIKA MKONDO WA NUNGWI .

AMESEMA KUWA KUFUATIA HALI HIYO WALIFANYA MAWASILIANO NA VYOMBO KADHAA KUOMBA MSAADA NA NDIPO ZILIPOFIKA BOTI MBILI ZA KMKM NA BOTI YA SKAGITI KWA AJILI YA KUSAIDIA.

AMEONGEZA KUWA ILIPOFIKA SAA 11.17  MASHINE MOJA YA BOTI HIYO ILIENDELEA KUFANYA KAZI NA  KUANZA SAFARI YAKE  KUELEKEA UNGUJA AMBAPO ILIFIKA SALAMA.

AIDHA KATIKA HALI YA KUSHANGAZA KAPTAINI WA MELI HIYO NDUGU MORIS SABINI HAKUWEZA KUPATIKA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VYOMBO MBALIMBALI VILIVYOKUWA VIKIMUHITAJI NA BADALA YA KUAMBIWA NA WAFANYAKAZI WA BOTI  HIYO KWAMBA AMETOKA NJE YA BANDARI.

MIONGONI MWA TAASISI ZILIZOKUWA ZIKIMUHITAJI KUFANYA MAZUNGUMZO NAYE KUFAHAMU KWA KINA CHANZO CHA MKASA HUO NI PAMOJA NA MAMLAKA YA USAFIRISHAJI YA ZANZIBAR AMBAPO MAAFISA WA TAASISI HIYO WALIELEZWA KWAMBA KAPTAINI HAYUPO.

ABIRIA WALIOZUNGUMA NA ZBC WAMESEMA KUWA HALI ILIKUWA MBAYA KUFUATIA KUZIMA MOTO KWANI HIYO SIYO MARA YA KWANZA KUTOKEA KADHIA YA AINA HIYO KATIKA KIPINDI CHA WIKI MOJA.

WAMEFAHAMISHA KUWA KATIKATI YA WIKI HII BOTI HIYO  ILIZIMA MOTO KWA KIPINDI CHA ROBO SAA  IKITOKEA BANDARI YA UNGUJA JAMBO LINALOTIA MASHAKA KWAMBA BOTI HIYO NI MBOVU NA KUNAHITAJIKA KUFANYIKA UCHUNGUZI WA KINA KUFAHAMU KWA NINI INAFANYA SAFARI ZAKE NA HALI HAINA UZIMA WA KUSAFIRI.

Advertisements