Naibu waziri wa afya Dr. Sira Ubwa Mwamboya

Wizara ya afyaZanzibarimewataka wamama wajawazito kuendelea kuchangia huduma za afya kwa njia ya upasuwaji na kawaida hadi bajeti ijayo itakayoanza Julai mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari naibu waziri wa wizara hiyo Dr. Sira Ubwa Mwamboya amesema tamko la rais wazanzibarn Dr. Ali Mohammed Shein la kuitaka wizara hiyo kuondoa uchangiaji wa huduma huduma hizo haliwezi kutekelezwa katika kipindi hichi kutokana na ukosefu wa bajeti.

Amesema katika kutekeleza tamko hilola rais alilotoa katika ziara yake ya mkoa wa Kusini Unguja linahitaji maandalizi ya msingi ikiwemo dawa na vifaa zinazohitaji bajeti mpya

        Aidha Dr. Sira amesema kutokana na hali hiyo amewaomba wananchi kuwa na subra katika utekelezaji wa mpango huo na kuwataka kuendelea kuchangia huduma hizo.

Katika ziara hiyo Dr. Shein aliitaka wizara ya afya kuondoa michango ya utowaji wa huduma za uzazi kwa njia ya upasuwaji na kawaida kwa mama wajawazito.

Awali wizara ya afya inawachangisha mama wajawazito wanaojifungua kwa njia ya upasuwaji kuchangia shilingi elfu 40 na wanaojifungua kwa njia ya kawaida huchangia vifaa.

Katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja zaidi ya mama wajawazito 40 huzalishwa kwa njia ya upasuwaji.

Advertisements