Juma Ali Khatib

Benerd Membe

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kuanza taratibu za kudai fedha za fidia za malipo ya rada ya ulinzi iliyolipwaTanzania na kampuni ya kimataifa ya B.AE System nchini Uingereza.

Akizungumza Zanzibar Islamic Blog katibu mkuu wa chama cha TADEA Juma Ali Khatib amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapaswa kuzidai fedha kwa vile ni haki ya walipa kodi waZanzibarkwa mujibu wa katiba.

Amesema Zanzibar imekuwa ikichangia mambo mengi ya muungano pamoja na unuzi wa rada hiyo .

 Taarifa hiyo ya TADEA inakuja kufuatia waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Benard Membe hivi karibuni kutangaza fedha hizo zitatumika katika sekta ya elimu ya msingi na kilimo hukoTanzania bara.

  Serikali ya ya muungano itapatiwa zaidi ya shilingi bilioni 75 kupitia akaunti ya benki kuuTanzania kama fidia ya ununuzi wa rada kutoka kampuni ya B.A.E System iliyodaiwa kukiuka taratibu za biashara ya kimataifa wakati ilipouza rada hiyo.

Waziri Membe amesema Serikali ya Uingereza na Serikali ya Tanzania zilijadiliana na kukubaliana kuwa fedha hizo za wananchi wa Tanzania zirejeshwe kupitia Serikali ya Tanzania na kwamba, serikali hizo mbili (ya Uingereza na Tanzania), zilikubaliana kuwa fedha hizo zitumike kwenye sekta ya elimu.

Alisema katika mpango huo, serikali ilidhamiria kutumia fedha hizo kununua vitabu milioni 4.4 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi nchini na pia kununua vitabu 192,000 vya kufundishia kwa ajili ya walimu wa shule za msingi

Advertisements