DR. ALI MOHAMMED SHEIN

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein amesema serikali itawajibisha mawaziri waliotajwa kuhusika na ufisadi na kamati teule ya baraza la wawakilishi baada ya kufanyia kazi tarifa hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari ikulu mjini Zanzibar amesema serikali hivi sasa inaifanyia kazi ripoti hiyo iliyowahusisha baadhi ya mawaziri wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na tuhuma za ufisadi.
Dr. Shein amefahamisha kuwa baada ya kuifanyia kazi taarifa hiyo serikali itaamua juu ya hatma ya mawaziri hao na viongozi wengine wa taasisi za serikali na mashirika ya umma wanaodaiwa kufanya ubadhirifu wa mali za umma kwa kutumia nyadhifa zao
Kuhusu matatizo ya muungano Dr. Shein amesema Zanzibar imeamuwa kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia kwenya orodha ya mambo ya muungano ambalo amesema litapatiwa muafaka.
Ameyataja baadhi ya mambo mengine yanayodaiwa na Zanzibar kwenye muungano, ni ushiriki wa Zanzibar katika shirikisho la jumuiya ya Afrika mashariki, ushirikiano wa kimataifa, ajira za taasisi za muungano, uwezo wa kukopa katika taasisi za kimataifa pamoja na kuwa na taasisi moja ya kukusanya kodi.
Dr. Shein amesema mambo hayo yanayodaiwa na Zanzibar kwenye muungano hayana uhusiano na mabadiliko ya katiba mpya kwa vile, yanaendelea kudaiwa kupitia vikao vya kero za muungano.
Hata hivyo Dr. Shein amewataka wananchi kutoa maoni yao juu ya mabadiliko ya katiba mpya ya muungano, katiba ambayo itasaidia kupunguza kero za muungano.
Mkutano huo wa Dr. Shein unaofanyika kila baada ya miezi mitatu kuzungumzia utekelezaji wa shughuli za serikali pia ulihudhuriwa na makamo wa kwanza wa rais Zanzibar Malims Seif Sharif Hamad

Advertisements