Amir Mkuu wa jumuiya ya UAMSHO Shekh Farid Adi Ahmed

Junuiya ya mihadhara ya kislamu Uamsho imekanusha kuhusika na  vurugu zilizotokea hivi karibuni kwa kuchomwa moto makanisha na kuvujwa kwa mabaa.

Akizungumza na wandishi wa habari Amir Mkuu wa jumuiya hiyo shekh Farid Adi Ahmed huko msikiti wa Mchangani Mjini Zanzibar, amesema kitendo hicho hakikufanywa na jumuiya hiyo kwani inamini uislamu unakataza kumbagua mtu kwa dini yake au maumbile yake.

Sheikh Farid amesema baadhi ya majina ya watu waliohusika katika matukio hayo wanayo, lakini wanaendelea kuyafanyia uhakiki ili kuyapaleka katika vyombo vya sheria

Hata hivyo amesema matukio hayo yamepandwa na kikundi cha watu wachache wasioitakia mema Zanzabar.

Aidha Sheikh Farid amekanusha madai kwamba jumuiya hiyo inafadhiliwa kutoka nje ya nchi.

Amesema jumuiya hiyo inaendeshwa kwa michango ya wafuasi wake wakati wa kuendesha mihadhara

Advertisements