Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohammed Aboud

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema itawanyanganya vitambulisho vya Uzanzibari Ukaazi watu na wageni waliopewa vitambulisho hivyo kinyume na sheria.

        Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohammed Aboud amesema kabla kufikia hatua hiyo serikali itafanya utafiti ili kujua idadi ya watu hao na wageni waliopewa vitambulisho vya ukaazi kinyume na sheria.

        Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi, amesema watendaji waliotoa vitambulisho hivyo kwa kuwapa watu wasiostahiki watachukuliwa hatua kali za sheria kutokana na kutumia madaraka vibaya.

Amesema baadhi ya wageni waliopatiwa vitambulisho hivyo wamehodhi nafasi za ajira zinazostahiki kupewa wazanzibari kwa kujitambulisha wakaazi

        Aidha waziri Aboud amesema serikali itaendelea kuwapatia vitambulisho vya ukaazi wazanzibari waliokoseshwa vitambulisho hivyo kwa sababu mbali mbali zikiwemo za kisiasa

Advertisements