Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeombwa kuunda tume kuwachunguza watendaji wake kutokana na kutapakaa kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali za umma.

Akichangia hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka 2012/2013 mwakilishi wa jimbo la Dole Shawana Bukheit Hassan amesema tume hiyo itasaidia kujua uhalali wa raslimali za viongozi hao kulingana na mapato yao.

 Shawana amesema fedha serikali zinazokusanywa zinaishia mikononi mwa watendaji wa serikali, hivyo kuundwa kwa tume kutasaidia kupunguza ubadhirifu wa mali za umma

        Nae mwakilishi wa jimbo la Kojani Hassan Hamad Omar ameiomba serikali kuwajibisha viongozi wanaobainika kufanya ubadhirifu.

        Akichangia hotuba ya bajeti amesema baadhi ya viongozi wamekua wakionewa muhali kuwajibisha huku wakiendelea kufanya ubadhirifu wa fedha za umma katika sekta za uchumi

Advertisements