Tanzania imegundua malimbikizo ya gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 20.97 katika maeneo ya ukanda wa pwani, ambayo yamekuwa yakitafutwa katika bahari kwa miaka mitatu sasa.

Waziri wa nishati na madini Sospiter Muhongo, amesema mbali ya kiwango hicho pia kimegunduliwa kisima cha gesi kiitwacho Lavani.

 Ugunduzi huo umefanywa na kampuni ya Statoil and Exxon Mobil ya Norway kilomita 80 kutoka pwani ya mkoa wa Lindi.

Waziri huyo pia amesema kwa miaka mitatu iliyopita shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta zimekuwa zikifanyika ambapo juhudi zilikuwa zikielekezwa zaidi katika maeneo ya kina cha bahari ya Hindi

 

Advertisements