Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka viongozi waliondolewa  madarakani wakiwemo mawaziri wa zamani kuhama katika nyumba za serikali ili kuwapisha mawaziri wa sasa.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi naibu waziri  wa ardhi, makaazi, maji na nishati Haji Mwadini Makame amsema badhi ya mawaziri wamelazimika kuishi katika nyumba za kukodi kutokana na mawaziri wa zamani kungania kuishi katika nyumba za serikali.

Hivyo amewaomba viongozi waliomaliza muda wao madarakani kuhama katika nyumba za serikali ili kuwapa fursa viongozi wa sasa kuishi katika nyumba hizo

Advertisements