Waziri wa katiba na sheria Zanzibar Abubakar Khamis Bakar amesema jukumu la kuliondoa jina la serikali ya Mapinduzi na kuliweka Jamhuri ya watu waZanzibarlinaweza kufanyika kupitia kwa wananchi.

Waziri Bakar ametoa ufafunzi huo katika baraza la wawakilishi wakati akijibu suala la mwakilishi wa mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu alietaka kujua chombo kilichofuta jina la Jamhuri ya watu waZanzibarna kuliweka jina la serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Waziri huyo amesema jina la Jamhuri lilikuwa likitumika katika sheria ya katiba yaZanzibarnamba 5, ya mwaka 1964, lakini baada ya kufanyika muungano waTanganyikanaZanzibarApril 26 1964 na kundwa Jamhuri ya MuunganoTanzaniajinahilolilifutika kutokana na sheria za katiba zilizotumika.

Hata hivyo amesema kwa vile jina la Jamhuri ya watu wa Zanzibar halikufutwa kisheria ni rahisi kulirejesha tena pale endapo wazanzibari watataka kulirejesha

Advertisements