Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema imefikia hatua nzuri na nchi yaOmankuwapeleka vijana waZanzibarkwenye kufanyakazi za heshima katika nchi hiyo.

        Akijibu sauala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa kazi uwezeshaji wananchi kiuchumi Harouna Ali Suleiman amesema katika ziara yake nchi humo hivi karibuni amefanya mazunguzo na maafisa waOmanna kuonyesha moyo wa kuwapokea vijana waZanzibarkwenda kufanya kazi.

Kuhusu nchi yaQataramesema mkataba wa kwenda kufanyakazi nchini humo umesainiwa chini ya kivuli cha serikali ya muungano, lakini amesemaZanzibarinafanya utaratibu wa kusaini mkataba wake na nchi hiyo.

Aidha waziri Suleiman amesema katika bajeti ya mwaka huu serikali imetenga shilingi bilioni moja na milioni 100 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa ajira kwa vijana.

Amesema chini ya mpango huo serikali itawapatia vijana mafunzo ya ujuzi wa kujiajiri, kuanzisha vikundi vya ushirika na kupatiwa mikopo yenye masharti nafuu ya kujiendeleza kiuchumi

Advertisements