Madaktari katika hospitali za umma Tanzania bara wameanza mgomo unaoweza kupoteza maisha ya wagonjwa.

        Mgomo huo ulioanza mwishoni mwa wiki tayari umesababisha huduma za matibabu kuanza kudhorota katika baadhi ya hospitali za serikali.

        Kiongozi wa kamati iliyoandaa mgomo wa madaktari Dr. Ulimboka Steven amesema mgomo huo umekuja baada ya serikali kushindwa kutekeleza madai yao kwa kipindi cha siku 90 zilizopita.

        Amesema madaktari wanadai kuimarishiwa maeneo ya kazi ikiwemo upatikanaji wa vifaa na maslahi bora……

Mgomo huo ambao ni wa pili kutokea katika kipindi cha mwaka huu unaweza kuleta athari kubwa kwa wagonjwa na wengine wanaweza kupoteza maisha ikiwa hautapatiwa ufumbuzi

Advertisements