Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema haitaivumilia SOBA houses yeyote ambayo itadaiwa kuhusika na matumizi ya dawa ya kulevya ndani ya nyumba hizo.

        Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa kwanza wa rais Fatma Abdulhabib Fereji ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Migombani.

        Amesema kuna madai ya baadhi ya SOBA house zinauza dawa za kulevya kwa vijana wanaoishi ndani ya nyumba hizo kwa wakiwa na lengo la kuachana na utumiaji wa dawa hizo

        Akizungumzia juu ya maadhimisho ya kupinga siku ya dawa za kulevya duniani waziri Fatma amesema bado tatizo la dawa za kulevya ni kubwa na juhudi za pamoja zinahitajika ili kupambana nalo.

        Amesema tabia iliojengeka ya usiri wa kuchelea lawama kwa wahusika linaleta athari kubwa kutokana na vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wanaendelea kuathirika na dawa hizo.

        Siku ya kimataifa ya upigaji vita matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya duniani inaadhishwa kila ifikapo June 26 ya kila mwaka na ujumbe wa mwaka huu ni tujenge jamii yenye afya

Advertisements