Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepinga kuwepo kwa mgomo baridi wa Madaktari wa Zanzibar katika hospitali za umma wanaodai maslahi yao kama ilivyo kwa madaktari wa Tanzania bara.

Waziri wa nchi ofisi ya rais, utumishi wa umma na utawala bora Haji Omar Kheir amesema hakuna mgomo wa aina yoyote uliofanywa na madaktari wa Zanzibar wa kudai maslahi yao.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema baadhi ya maslahi wanaodai madaktari hao yakiwemo posho la nyumba na likizo wamepatiwa tokea mwezi Mei mwaka huu na maslahi mengine watalipwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013.

Aidha waziri Kheir amesema serikali imepandisha mishahara kwa wataalamu ikiwemo kada ya madaktari waliongozewa posho la nyumba, mazingira ya hatari kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Advertisements