Wananchi wa Zanzibar waliokoseshwa vitambulisho vya ukaazi wameshauriwa kuishtaki serikali kwa kuwakosesha haki hiyo na kuwapatia wagenzi wasiostahiki.

Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya nchi ofisi ya rais na baraza la Mapinduzi mwakilishi wa jimbo la Ziwani Rashi Seif amesema kwa zaidi ya miaka mitano sasa suala hilo limekuwa likilalamikiwa, lakini serikali haijachukua hatua yoyote.

Hivyo ni vyema kwa wanachi kuchukua uwamuzi wa kuipeleka mahakamani serikali ili kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi

Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi Mohammed Juma akimfahamisha jambo rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Sehin (kushoto) kuhusu vitambulisho hivyo.

Wawakilishi wengine waliochangia hotuba hiyo wameishauri serikali kuunda tume ya kuchanguza suala la baadhi ya wananchi kunyimwa vitambulisho vya Mzanzibar ukaazi na kupewa wageni.

Wamesema tatizo la wananchi kukoseshwa vitambulisho hivyo ni kubwa hivyo iko haja kwa serikali kuunda tume itakayochunguza chanzo cha tatizo hilo na baadae kupatiwa ufumbuzi.

Wamesema vitambulisho vya ukaazi ni haki ya mzanzibari mwenye sifa ikiwemo kutimiza miaka 18, lakini baadhi yao wamekuwa wakinyimwa kwa sababu za kibinafsi na kupatiwa wageni haki hiyo wageni.

Hata hivyo wajumbe hao wamewatupia lawama baadhi ya masheha ni miongoni mwa viongozi wa serikali za mitaa wanaochangia kuwakosesha wananchi vitambulisho vya ukaazi na kuwapatia wageni.

Advertisements