Wizara ya afya Zanzibar imesema pamoja na juhudi zinazochukuliwa na serikali kuwaelimisha wananchi juu ya athari ya maradhi ya ukimwi, bado maambukizi ya virusi vya ukimwi yanazidi kuenea.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 waziri Juma Duni Haji amesema maradhi ya ukimwi bado ni tishio kwa jamii hivyo iko haja   kwa wananchi kuchukua tahadhari zaidi.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 watu elfu moja, 774 waligundulikwa kuwa na virusi vya ukimwi wakiwemo wanawake elfu moja na 90 kati ya watu elfu 87, 306 waliopima virusi vya ukimwi Unguja na Pemba

Kuhusu matengenezo ya chumba cha wagonjwa mahtuti katika hospitali ya Mnazi mmoja, Duni amesema matengenezo hayo yako katika hatua za mwisho ya uwekaji mtandao wa hewa ya oxygen.

Amesema kazi hizo zinafanywa na kampuni ya tanzania oxygen limeted zinatarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu ambapo serikali ya mapinduzi Zanzibar imetumia zaidi ya shilingi milioni 500.

Wizara ya afya katika bajeti ya mwaka 2012/2013 imeomba kudhinishiwa zaidi ya shilingi bilioni 40 na milioni 216 kwa kazi za kawaida na maendeleo

Advertisements