Mansour Yussuf Himid

Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Mansour Yussuf Himid amesema wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na muungano unaozingatia utaifa wa pande zote mbili ikiwemo kutambuliwa kimataifa.

Amesema hakubaliani na mfumo wa mungano uliopo sasa kutokana na Zanzibar kunyimwa fursa za kumiliki uchumi, kutambuliwa na umoja wa mataifa pamoja na kupata nafasi ya kujiunga na taasisi za kimataifa.

Akichangia  hotuba ya bajeti ya wizara katiba na sheria Zanzibar katika kikao cha baraza la wawakilishi Mimid amesema asilimia 4.5 ya misaada ya nje inayopata Zanzibar ni ndogo, hivyo iko haja kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni juu ya katiba mpya ili muungano uliopo uwe na maslahi kwa Zanzibaar

Nae mwakilishi wa jimbo la Uzini Mohammedraza Hassanal amesema muungano wa Tanganyika Zanzibar ni muungano wa kihistoria, lakini Zanzibar kama nchi ilipaswa kuona mkataba wa muungano huo.

Amesema hatua hiyo itavisaidia vizazi vijavyo kujua historia ya muungano, lakini amedai baadhi ya mambo yaliongizwa kutoka 11 hadi 22 hayana saini ya viongozi wa Zanzibar

Advertisements