Baadhi ya abiria waliotoka nje ya meli ya Mv Sky Get kabla ya kubirukia katika eneo la bahari ya Chumbe.

MELI NDOGO YA ABIRIA NA  MIZIGO YA MV. SKY GET INAYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA SEA GUL IMEZAMA JANA MCHANA IKIWA NA ZAIDI YA ABIRIA 390.

MELI HIYO IMEZAMA JANA WAKATI IKITOKEA BANDARI YA DAR ES SALAAM KUJAZANZIBAR KATIKA ENEO LA KISIWA CHA CHUMBE UNGUJA.

           HADI KUFIKIA LEO ASUBUHI ZAIDI YA WATU 100 WAMEOKOLEWA WAKIWA HAI NA MAITI 31 ZIMEPATIKANA AKIWEMO MTALII MMOJA AMBAE URAI WAKE HAUJFAHAMIKA.

 SHUGHULI ZA UKOZI BADO ZINAENDELEA, LAKINI KWA MUJIBU WA WAOKOZI HAWATEGEMNEI KUWAPATA WATU WAKIWA HAI KUTOKANA NA HALI MBAYA YA HEWA IKIWEMO BARADI KALI.

 KUFUATIA MSIBA HUO SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMETANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBELEZI KUANZIA LEO NA BENDERA ZOTE ZITAPEPEA NUSU MLINGOTI.

AIDHA SEERIKALI IMESEMA ITAGHARAMIA SHUGHULI ZOTE ZA MAZISHI ZA WATUWALIOKUFA KWENYE MELI HIYO PAMOJA NA KUWAPATIA MSAADA WALE WALIONUSURIKA.

AKITOA TAARIFA HIYO RAIS WA ZANZIBAR NA MWENHYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR. ALI MOHAMMED SHEIN AMEWATAKA WANANCHI NA JAMAA WA WAATHIRIKA HAO KUWA WASTAHAMILIVU NA WATULIVU KATIKA KIPINDI HIKI CHA MSIBA.

INSPETA GENERAL WA POLISI SAID MWEMA AMESEMA JESHILI LA POLISI INAENDELEA NA UCHUNGUZI WA CHANZO CHA AJALI HIYO TANGU ILIPOONDOKA BANDARINI HADI KUZAMA.

AMESEMA JESHI LA POLISI PIA LITAONGEZA NGUVU KATIKA SHUGHULI ZA UOKOZI WA MELI HIYO.

HII NI MELI YA PILI KUZAMA NA  KUPOTEZA WATU WENGI KWA WAKATI MMOJA AMBAPO SEPTEMBA MWAKA JANA MELI YA MV. SPICE ISLANDER ILIYOKUWA IKITOKEA BANDARI YA MALINDI UNGUJA KUELEKEA KISIWANI PEMBA ILIZAMA KATIKA MKONDO WA NUNGWI NA ZAIDI YA WATU 2000 WAMEPOTEZA MAISHA YAO.

WATAALAMU WA MASUALA YA BAHARI WANADAI VYANZO VYA AJALI HIYO KINATOKANA NA UCHAKAVU WA MELI, UDOGO WA KUTOHIMILI VISHINDO VYA BAHARI PAMOJA NA KUTOFUATA SHERIA ZA USAFIRI WA BAHARINI IKIWEMO KUONGEZA IDADI YA ABIRIA NA MIZIGO.

AIDHA VYOMBO HIVYO VINADAIWA KUWA NA UHABAR WA VIFAA VYA UKOZI VIKIWEMO LIFE JACKE PAMOJA NA VIKOSI VYA UKOZI VYA SERIKALI KUKAWIA KUFIKA KATIKA ENEO LA TUKIO KUTOKANA NA UKOSEFU WA VIFAA VYA UKOZI.

 

 

Advertisements