Eneo la bustan ya Forodhan Zanzibar

Wizara ya nchi ofisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi kupitia baraza la manispaa linatarajia kuingia awamu ya pili ya ujenzi wa uzio wa Bustani ya Forodhani ili kuliweka eneo hilo katika mazingira mazuri

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa wizara hiyo Dr. Mwinyihaji Makame amesema serikali kwa kushirikiana na Benki ya dunia imekamilisha taratibu za kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi huo.

Kuhusu ulinzi wa bustani hiyo ambao kwa sasa hauridhishi Dr. Makame amesema hali hiyo inatokana kufuatia kumaliza muda wa mkataba wa msaada wa fedha kutoka Jumuiya ya  Aga Khan Foundation kumaliza.

Amesema awali bustani hiyo ilikuwa ikilindwa na kampuni ya ulinzi ya K.K Security, lakini hivi sasa inashughulikiwa na bodi maalum na kukiri kuwepo kasoro za utendaji katika usimamizi wa bustani hiyo

Busatani ya Forodhani iliofanyiwa matengenezo ya awamu ya kwanza mwaka 2008 inakusanya zaidi ya shilingi milioni 40 kwa mwezi kupitia ada wanazotozwa wafanyabiashara katika eneo hilo.

Advertisements