Ali Ameir Mohammed

Mbunge wa zamani wa jimbo la Donge Ali Ameir Mohammed amewataka wananchi kutafakari juu ya udugu wa damu na muingiliano wa raslimali zao ndani ya jamhuri kufuatia kuwepo kauli za kutaka kuvunja muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema matatizo ya muungano yanazungumzika na kupatiwa ufumbuzi, lakini amani na utulivu iliopo iliyochangiwa na muungano haiwezi kurejesheka katika kipindi kifupi.

Hivyo ni vyema kwa wananchi kutofikiria dhana ya kuuvunja muungano na kutaka kupuzwa vikundi vya watu wachache wenye lengo la kukataa muungano kwa maslahi yao binafsi

Kauli za mwanasiasa huyo kutoka chama cha Mapinduzi CCM zinakuja wakati huu baadhi ya viongozi wa chama hicho wakidaiwa kukiuka sera za chama chao za mfumo wa muungano wa serikali mbili.

         mambo ya ndani na naibu katibu mkuu wa CCM, Zanzibar amekanusha uvumi uliosambazwa kwa ujumbe mfupi wa njia za simu kuwa amefariki dunia.

        Amesema wanaosambaza uvumi huo ni wale wasiomtakia mema na kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi

        Hii ni mara ya pili kwa mwanasiasa huyo kusingiziwa amefariki dunia ambapo mara ya kwanza miaka miwili iliyopita alisingiziwa amekufa wakati alipokwenda matibabuni nchini China.

 

Advertisements