Waziri Mohammed Aboud

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeomba radhi kufuatia baadhi ya mabalozi wa nchi za kiarabu waliopo Zanzibar kuzuiliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amani Abeid Karume mjini Zanzibar.

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohammed Aboud amesema serikali itawahakikishia mabolozi waliopo Zanzibar na kutoka nchi nyingine kitendo kama hicho hakitatokea tena.

Amesema wafanyakazi waliofanya vitendo hivyo watashughulikia ili kuona heshma na nidhamu inaendelea kuwepo kwa viongozi hao wa kimataifa walioletwa na nchi zao kudumisha ushirikiano

Awali mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma alitishia kuzuwia kifungu cha fedha cha wizara ya miundo mbinu na mawasiliano wakati wakupitisha bajeti ya wizara hiyo akitaka serikali kutoa kauli juu ya kitendo cha kufungiwa geti maafisa hao wa kibalozi katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.

Hata hivyo Juma ameitaka serikali kuheshimu sheria katika uteuzi wa viongozi wa mamlaka za taasisi za serikali badala ya kutumia utashi binafsi

Advertisements