Waziri wa fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajiwa kubana matumizi ya kazi za kawaida katika bajeti ya mwaka 2012/2013 ili kuchangia mfuko wa fedha za ununuzi wa meli mpya ya abiria na mizigo.

        Akiwasiisha hotuba ya bajeti ya wizara ya nchi ofisi ya rais fedha, uchumi na mipango ya maendeleo, Omar Yussuf Mzee amesema mpango huo wa serikali ni kutaka kuondoa usumbufu wa usafiri wa baharini unaolalamikiwa na wanachi

Amesema hatua nyingine itakayochukuliwa katika ununuzi wa meli hiyo ni kuongeza kiwango cha mkopo wa ndani kutoka benki ya watu wa Zanzibar PBZ na mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF.

Mzee amesema shilingi milioni 40 katika idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa Zanzibar wanaioshi nchi za nje zitaondolewa na kuingizwa kwenye mfuko mkuu wa serikali ili kusaidia ununuzi wa meli hiyo

Hatua hiyo ya wizara ya fedha kubana matumizi ya kazi za kawaida imekuja kufuatia agizo la rais Dr. Ali Mohammed Shein kuitaka wizara hiyo kutafuta fedha za kununua meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria elfu moja na tani 100 za mizigo.

Advertisements