Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imezuwia utowaji wa leseni za biashara kwa muda wa miaka mitatu sasa kwa wafanyabiashara katika eneo la Jua kali Darajani kutokana na eneo hilo kuzuiliwa na mahakama.

        Kauli hiyo ya serikali imekuja kufuatia baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kutaka kuzuwia vifungu vya bajeti ya wizara ya biashara, viwanda na masoko juu ya kutopewa leseni wafanyabiashar wa eneo hilo.

Waziri wa nchi ofisi ya rais na baraza la Mapinduzi Dr. Mwinyihaji Makame amesema eneo hilo limetengwa kwa ajili shughuli nyingine ikiwemo bustani ya mapumziko na sio biashara.

Amesema serikali kupitia baraza la manispaa haiwezi kuingilia kati uwamuzi wa mahakama kwa kuwaruhusu wafanyabiashara hao kufanya biashara katika eneo hilo na kuwataka kulitumia eneo la Saateni….

Wakati huo huo serikali imesema itaendelea kudhibiti bidhaa zinazopunguziwa  kodi ili kuuzwa kwa bei nafuu nchini hazitoroshwi kwenda kuuza nchi nyingine.

Dr. Makame amesema serikali imeondoa ushuru wa uingizaji wa vyakula kama vile mchele, unga wa ngano na suakari ili kuona wananchi wanapata nafuu ya bei katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan

Advertisements