Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeombwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya muungano yanayolalamikiwa na Zanzibar kabla ya kuanza kwa katiba mpya ya Jamhuri ya muungano Tanzania.

        Mwakilishi wa kuteuliwa Ali Mzee Ali amesema taasisi kama vile benki kuu BOT, mamlaka ya mapato Tanzania TRA na taasisi nyingine zinalalamikiwa na upande wa pili wa muungano kwa madai ya kukwamisha maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.

        Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya fedha, uchumi na mipango ya maendeleo katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema muundo wa taasisi hizo haziko katika mfumo wa muungano na kusababisha matatizo kutokana na utendaji wake kufimbiwa macho na serikali zote mbili.

        Hivyo ameiomba serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia vikao vya kutatua kero za muungano kuyapatia ufuimbuzi matatizo hayo kabla ya kuanza kwa katiba mpya

Nae mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma ameiomba serikali kuingilia kukwama kwa zaidi ya gari 500 za wafanyabiashara wa Zanzibar katika bandari ya Dar es Salaam.

        Amesema tatizo la wafanyabiashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili limechangia kukwama kwa gari hizo, hivyo iko haja ya kwa serikali kulipatiwa ufmbuzi wa haraka.

Advertisements