Jumuiya ya taasisi za dini ya kilamu Zanzibar leo zimendesha dua ya pamoja ya kuiombea nchi kuwa na amani na utulivu katika msikiti wa masjidi Shurba, Kidongochekundu wilaya ya Mjini.

Dua hiyo ilimbatana na uchinjaji wa ngombe saba, mbuzi 33 na kuku kadhaa kwa ajili ya kutoa sadaka ya kuwaombea waumini wa dini ya kislamu waliokumbwa na kadhia ya upigwaji wa mabomu siku zilizopita.

Miongoni mwa viongozaji wa dua hiyo Sheikh Mussa ambayo ilihudhuriwa na mamia ya waumini wa kislamu kutoka maneo mbali mbali ya mji wa Zanzibar na baadhi ya vijiji vya karibU

        Wiki mbili zilizopita jumuiya ya Uamsho ilifanya ibada ya kuwaombea dua wananchi waliozama kwenye meli ya Mv. Skagit, lakini dua hiyo ilingiliwa kati na jeshi la polisi kwa madai ya kufanya mkusanyiko uliokuwa hauna kibali.

Advertisements