Eneo la Bandari ya Dar es Salaam

Waziri wa biashara, viwanda na masoko Nassor Ahmmed Mazurui amewataka wafanyabiashara wanaotozwa bidhaa zao kodi mara mbili Tanzania bara kuwasilisha nyaraka za ulipishwadi wa kodi hizo ili wizara ichukue hatua za kisheria.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema licha ya suala hilo kupatiwa ufumbuzi katika vikao vya kutatua kero za muungano, lakini malalamiko hayo bado yanaendelea.

Hivyo amesema kuwasilishwa kwa nyaraka hizo wizara itajenga hoja ya majadiliano ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo la muda mrefu

Aidha Marzui amesema serikali bado inakabiliwa na tatizo la kuwaendeleza wajasiriamali ili kuwawezesha kuzalisha kwa tija na kupambana na umasikini.

Amesema shilingi milioni 200 zilizoahidiwa na rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kwaendeleza wajasiriamali wa Zanzibar bado fedha hizo hazijapatikana na wizara yake inaendelea kuzifuatilia.

Mazurui amesema wizara itakapozipata fedha hizo zitatumika katika maeneo ya ununuzi wa vifaa, ufunganishaji wa bidhaa, utambulisho wa bidhaa pamoja na mafunzo.

Wizara ya biashara, viwanda na masoko imeombea kuidhinishwa zaidi ya shilingi bilioni tano na milioni 580 kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Advertisements