Archive for October, 2012

JUSSA ATAKA KUJIUZULU

 

Ismail Jussa Ladhu

Leo asubuhi nimewasilisha kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba barua ya kuomba kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) kwa upande wa Zanzibar, uamuzi ambao nimeomba uanze kutekelezwa rasmi tarehe 10 Oktoba, 2012.

 

Nimechukua uamuzi huu baada ya kuzungumza na kushauriana na viongozi wangu wa juu wa Chama ambao ni Mwenyekiti, Profesa Lipumba, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Machano Khamis Ali na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad takriban miezi miwili iliyopita. Nawashukuru baada ya kunitaka niwape muda wa kulitafakari walinikubalia lakini wakaniomba nibakie hadi tutakapokamilisha baadhi ya shughuli muhimu za Chama katika kipindi hichi.

 

Sababu kubwa zilizonisukuma kukiomba Chama kiniruhusu niachie nafasi hii ni kutokana na muda mrefu sasa kuhisi kwamba majukumu niliyo nayo ya kuwa msimamizi mkuu wa utendaji wa Chama kwa upande wa Zanzibar na wakati huo huo kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe hakunipi fursa ya kujifaragua na kutumikia nafasi zote mbili kwa ufanisi unaotakiwa. Nataka kuona kazi ya kuibana Serikali ndani na nje ya Baraza ili iwajibike zaidi kwa wananchi inaimarika zaidi.

 

Sambamba na sababu hiyo ni kwamba nimekusudia kutumia muda mwingi zaidi kutoa mchango mkubwa zaidi katika harakati za wananchi wa Zanzibar zinazoendelea za kuhakikisha kuwa Zanzibar inarejesha mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na kuwepo kwa Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.

 

Harakati zinazoendelea Zanzibar kwa njia za amani na za kidemokrasia kwa kutumia mchakato wa Katiba Mpya zinahitaji kuungwa mkono na kupewa msukumo wa dhati na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar kwenda kusimamia maslahi yao na ya nchi yao. Nimetafakari na kuona kwamba nikiwa sina majukumu mengine ya kiutendaji nitakuwa na muda kutosha wa kulifanya hili mimi na Wawakilishi wenzangu tunaotoka CUF na CCM, vyama viwili vya siasa vilivyomo Barazani.

 

Nafurahi kwamba leo nimetimiza azma yangu hiyo. Pamoja na uamuzi huu, naendelea kubaki kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa. Nawahakikishia viongozi na wanachama wenzangu wa CUF kwamba tutaendelea kushirikiana pamoja katika shughuli nyengine zote za kisiasa za Chama na kwa pamoja tutafanya kazi kuyatimiza malengo tuliyojiwekea. Naahidi kumpa ushirikiano kikamilifu mwanachama yeyote atakayeteuliwa kujaza nafasi ninayoiwacha.

 

HAKI SAWA KWA WOTE

 

 

ISMAIL JUSSA

Zanzibar

05 Oktoba, 2012

USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA ZANZIBAR OCTOBA 15

Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa Zanzbiar bw. Vuai Suleiman (katikati) akiwa na mratibu wa mtandao wa wandishi wa habari wa uhamasishaji wa kazi za usajili Zanzibar Salma Salma Said (kushoto)

KAZI ZA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANANCHI UPANDE WA ZANZIBAR ZINATARAJIWA KUANZA TAREHE 15 MWEZI HUU HADI MARCH MOSI MWAKA 2013 KATIKA WILAYA ZOTE ZA UNGUJA NA PEMBA.

AKIZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI HUKO WIRELESS, MKURUGENZI MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA ZANZIBAR BW. VUAI MUSSA SULEIMAN AMESEMA KAZI HIZO ZA USAJILI NA UTAMBUZI KWA WANANCHI ZITAANZA WILAYA YA KUSINI KUANZIA SAA 2.00 ASUBUHI HADI SAA 10.00 JIONI KWA MUDA WA SIKU KUMI.

AMESEMA WANANCHI WA WILAYA YA KATI WATAANZA USAJILI TAREHE 29 HADI TAREHE 09 MWEZI UJAO, WILAYA YA MAGHARIB TAREHE 12 HADI 23 MWEZI UJAO, WILAYA YA MJINI TAREREHE 26 HADI DISEMBA 07, KASKAZINI ‘B’ TAREHE 10 HADI 21 DESEMBA, KASKAZINI ‘A’ TAREHE 24 DESEMBA HADI TAREHE NNE JANUARI MWAKA 2013.

KWA UPANDE WA PEMBA WILAYA YA MKOANI USAJILI UTAANZA TAREHE 07 HADI JANUARI 18 MWAKA UJAO, MICHEWENI JANUARI 21 HADI FEBRUARI MOSI, WILAYA YA WETE TAREHE 04 HADI FEBRURY 15 NA WILAYA YA CHAKECHAKE TAREHE 18 HADI MARCH MOSI MWAKANI.

BW. SULEIMAN AMSEMA WATAKAOFANYIWA USAJILI HUO NI RAIA WA TANZANIA, WAGENI NA WAKIMBIZI WALIOTIMIA UMRI WA MIAKA 18 WAKIWA NA MOJA YA VITAMBULISHO VIKIWEMO UZANZIBARI UKAAZI, HATI ZA KUSAFIRIA, CHETI CHA KUZALIWA, LESENI YA BIASHARA NA UDEREVA, CHETI CHA KUMALIZIA MASOMO YA MSINGI AU SEKONDARI.

AMESEMA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA ZANZIBAR INAAMINI WANANCHI, VIONGOZI WA DINI, MASHEHEA NA WANASIASA WATATOA USHIRIKIANO KWA MAAFISA WA USAJILI WAKATAKAOFANYA USAJILI HUO KILA SHEHIA.

BW. SULEIMAN AMEWATAJA WATU AMBAO HAWATASAJILIWA NI WAGONJWA WENYE MATATIZO YA AKILI WASIOSOGELEKA NA WATU WANAOSUBIRI KUTEKELEZEWA HUKUMU YA KIFO.

KUHUSU WAFANYAKAZI WA TAASISI ZA SERIKALI WALIOKOSA KUSAJILIWA AWAMU YA KWANZA, MKURUGENZI HUYO AMESEMA WAFANYAKAZI WA MAMLAKA HIYO WATAPITA TENA KUWASAJILI WAFANYAKAZI HAO KATIKA TAASISI ZAO.

AMEZITAJA BAADHI YA FAIDA ZITAKAZOPATIKANA KATIKA VITAMBULISHO HIVYO NI KUPATA MIKOPO KATIKA TAASISI ZA FEDHA, KUPUNGUZA VITERNDO VYA UHALIFU, KUEPUKANA NA WATUMISHI HEWA, KUPUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI PAMOJA NA KURAHISISHA KUMILIKI HATI YA KUSAFIRIA.

KAZI ZA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA ZINAZOFANYWA TANZANIA NZIMA ZINATARAJIWA KUENDELEA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO.