Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa Zanzbiar bw. Vuai Suleiman (katikati) akiwa na mratibu wa mtandao wa wandishi wa habari wa uhamasishaji wa kazi za usajili Zanzibar Salma Salma Said (kushoto)

KAZI ZA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANANCHI UPANDE WA ZANZIBAR ZINATARAJIWA KUANZA TAREHE 15 MWEZI HUU HADI MARCH MOSI MWAKA 2013 KATIKA WILAYA ZOTE ZA UNGUJA NA PEMBA.

AKIZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI HUKO WIRELESS, MKURUGENZI MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA ZANZIBAR BW. VUAI MUSSA SULEIMAN AMESEMA KAZI HIZO ZA USAJILI NA UTAMBUZI KWA WANANCHI ZITAANZA WILAYA YA KUSINI KUANZIA SAA 2.00 ASUBUHI HADI SAA 10.00 JIONI KWA MUDA WA SIKU KUMI.

AMESEMA WANANCHI WA WILAYA YA KATI WATAANZA USAJILI TAREHE 29 HADI TAREHE 09 MWEZI UJAO, WILAYA YA MAGHARIB TAREHE 12 HADI 23 MWEZI UJAO, WILAYA YA MJINI TAREREHE 26 HADI DISEMBA 07, KASKAZINI ‘B’ TAREHE 10 HADI 21 DESEMBA, KASKAZINI ‘A’ TAREHE 24 DESEMBA HADI TAREHE NNE JANUARI MWAKA 2013.

KWA UPANDE WA PEMBA WILAYA YA MKOANI USAJILI UTAANZA TAREHE 07 HADI JANUARI 18 MWAKA UJAO, MICHEWENI JANUARI 21 HADI FEBRUARI MOSI, WILAYA YA WETE TAREHE 04 HADI FEBRURY 15 NA WILAYA YA CHAKECHAKE TAREHE 18 HADI MARCH MOSI MWAKANI.

BW. SULEIMAN AMSEMA WATAKAOFANYIWA USAJILI HUO NI RAIA WA TANZANIA, WAGENI NA WAKIMBIZI WALIOTIMIA UMRI WA MIAKA 18 WAKIWA NA MOJA YA VITAMBULISHO VIKIWEMO UZANZIBARI UKAAZI, HATI ZA KUSAFIRIA, CHETI CHA KUZALIWA, LESENI YA BIASHARA NA UDEREVA, CHETI CHA KUMALIZIA MASOMO YA MSINGI AU SEKONDARI.

AMESEMA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA ZANZIBAR INAAMINI WANANCHI, VIONGOZI WA DINI, MASHEHEA NA WANASIASA WATATOA USHIRIKIANO KWA MAAFISA WA USAJILI WAKATAKAOFANYA USAJILI HUO KILA SHEHIA.

BW. SULEIMAN AMEWATAJA WATU AMBAO HAWATASAJILIWA NI WAGONJWA WENYE MATATIZO YA AKILI WASIOSOGELEKA NA WATU WANAOSUBIRI KUTEKELEZEWA HUKUMU YA KIFO.

KUHUSU WAFANYAKAZI WA TAASISI ZA SERIKALI WALIOKOSA KUSAJILIWA AWAMU YA KWANZA, MKURUGENZI HUYO AMESEMA WAFANYAKAZI WA MAMLAKA HIYO WATAPITA TENA KUWASAJILI WAFANYAKAZI HAO KATIKA TAASISI ZAO.

AMEZITAJA BAADHI YA FAIDA ZITAKAZOPATIKANA KATIKA VITAMBULISHO HIVYO NI KUPATA MIKOPO KATIKA TAASISI ZA FEDHA, KUPUNGUZA VITERNDO VYA UHALIFU, KUEPUKANA NA WATUMISHI HEWA, KUPUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI PAMOJA NA KURAHISISHA KUMILIKI HATI YA KUSAFIRIA.

KAZI ZA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA ZINAZOFANYWA TANZANIA NZIMA ZINATARAJIWA KUENDELEA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO.

Advertisements