Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetakiwa kuunda tume ya kuchunguza utapeli uliofanywa na baadhi ya watendaji katika utowaji wa nafasi za ajira.

Akizungumza Zanzibar Islamic News katibu mwenezi wa chama cha AFP Abdalla Hassan amesema chama hicho kimepokea taarifa kwa baadhi ya vijana waliofanyiwa utapeli huo na kuwataka wanasheria kuwa karibu na suala hilo ili kukomesha vitendo vya rushwa.

Amesema ajira hizo zilizokuwa zikinadiwa mwaka uliopita katika taasisi za ulinzi za muungano na vikosi vya SMZ, lakini vijana hao hawakupatiwa huku wakitoa fedha nyingi…..CLIPS..(SAVED-

        Aidha amesema utapeli huo uliofanywa na watendaji hao kwa kutumia taasisi zao ni vyema wakaundiwa tume ili kuwachukulia hatua za kisheria.

Advertisements