IDDIMataifa wanachama  wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC yametakiwa kuwa makini juu ya mfumo na muundo wa sekta ya mafuta na gesi inayotarajiwa kuwa muhimili wa uchumi mpya kwa nchi hizo.

Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein katika hotuba yake iliyosoma na makamu wa pili wa rais Balozi Seif Ali Idd katika ufunguzi wa mkutano wa sita wa siku tatu wa Mataifa hayo mjini Arusha.

Amesema ukanda wa Afrika Mashariki unahitaji sauti ya pamoja katika muundo huo utakaowezesha sekta hiyo kuyanufaisha mataifa hayo.

Dr. Shein amesema wawekezaji na makampuni ya Kimataifa yanayojihusisha na sekta ya mafuta na gesi yanaweza kushajiika na mfumo mzima wa ukanda huu kutegemea zaidi sera na miundombinu.

Amesema idadi kubwa ya wawekezaji wameonesha nia ya kutaka kuwekeza katika Sekta ya Mafuta na Gesi ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Uganda na Kenya kugundulika kuwa na Mafuta na gesi.             Nae waziri wa Nishati wa Uganda Irin Muloni amesema uendeshaji wa sekta ya Mafuta katika ukanda wa mataifa ya Afrika Mashariki utaimarishwa kwa maslahi ya Mataifa hayo.

Advertisements